HAFLA YA MAKABIDHIANO YA MAGARI YA MRADI WA REGROW JIJINI DODOMA | MALUNDE 1 BLOG

Monday, May 24, 2021

HAFLA YA MAKABIDHIANO YA MAGARI YA MRADI WA REGROW JIJINI DODOMA

  Malunde       Monday, May 24, 2021

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi akizungumza katika halfa ya kukabidhi magari 9 kwa taasisi za TAWIRI, Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), Bodi ya Utalii (TTB) ,Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) ,Bonde la Mto Rufiji (RBWB) ,na Timu ya Uratibu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kwa lengo la kuimarisha utendaji kazi wa taasisi hizo katika shughuli za mradi wa REGROW. Makabidhiano hayo yalifanyika jijini Dodoma.
Mratibu wa Mradi , Aenea Saanya akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu kwenye hafla ya makabidhiano ya magari ya Mradi wa Regrow iliyofanyika jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi akikata utepe katika hafla ya makabidhiano ya magari ya mradi wa REGROW huku akishuhudiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa na mwakilishi wa Tawiri, Dkt. Wilfred Mareale.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi akimkabidhi funguo za gari mwakilishi wa TAWIRI, Dkt. Wilfred Mareale kwenye hafla ya makabidhiano ya magari ya mradi wa REGROW jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi ( katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi wa Taasisi baada ya kukabidhiwa funguo za magari kwenye hafla ya makabidhiano ya magari ya mradi wa REGROW jijini Dodoma.

(Picha zote na Gladys Lukindo- Afisa Habari, Wizara ya Maliasili na Utalii)
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post