WATAALAMU WA UREMBO 'KAHAMA GLAMOUR BEAUTY SALON' WASHIRIKI MAONESHO KAHAMA - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Thursday, May 27, 2021

WATAALAMU WA UREMBO 'KAHAMA GLAMOUR BEAUTY SALON' WASHIRIKI MAONESHO KAHAMA


Mkurugenzi wa Kahama Glamour Beauty Salon, Bi. Sharifa Mohammed  akionesha bidhaa original anazotumia kupamba maharusi kwenye maonesho ya wajasiriamali na wawekezaji Kahama.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Wataalamu wa Urembo maarufu Kahama Glamour Beauty Salon wameshiriki Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama yanayofanyika katika Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kilichopo Nyihogo Mjini Kahama.

Akizungumza na Malunde 1 blog iliyotembelea banda lake, leo Alhamis Mei 27,2021 Mkurugenzi wa Kahama Glamour Beauty Salon, Bi. Sharifa Mohammed amesema wanashiriki maonesho hayo yaliyoandaliwa na Taasisi ya GS1 Tanzania ili kutangaza biashara na kazi wanazofanya pamoja na kujifunza kutoka kwa wajasiriamali wengine.

“Kahama Glamour Beauty Salon tunapamba maharusi, tunasuka nywele aina zote, tunauza bidhaa mbalimbali za urembo, tunakodisha nguo za harusi, tunafanya Decoration ya Paper Flower katika matukio mbalimbali,tunauza mapambo ya ndani kama vile saa za ukutani pia tunafundisha kuhusu kazi tunazofanya”,amesema Sharifa

Kahama Glamour Beauty Salon inapatikana Nyihogo Kahama karibu na  Haliwa Restaurant , mawasiliano 0753846701 Instagram @Kahama Glamour Beauty Salon

Mkurugenzi wa Kahama Glamour Beauty Salon, Bi. Sharifa Mohammed  akionesha picha ya ukutani kwenye maonesho ya wajasiriamali na wawekezaji Kahama. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Kahama Glamour Beauty Salon, Bi. Sharifa Mohammed  akionesha gauni la harusi kwenye maonesho ya wajasiriamali na wawekezaji Kahama
Mkurugenzi wa Kahama Glamour Beauty Salon, Bi. Sharifa Mohammed  akionesha Paper Flower Decoration ambazo anatengeneza mwenyewe kwenye maonesho ya wajasiriamali na wawekezaji Kahama
Mkurugenzi wa Kahama Glamour Beauty Salon, Bi. Sharifa Mohammed  akionesha saa ya ukutani kwenye maonesho ya wajasiriamali na wawekezaji Kahama
Mkurugenzi wa Kahama Glamour Beauty Salon, Bi. Sharifa Mohammed  akionesha saa ya ukutani kwenye maonesho ya wajasiriamali na wawekezaji Kahama.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Soma pia:

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages