BENKI YA EXIM YATOA ZAWADIYA EID KWA WATOTO YATIMA DAR, MBEYA, SHINYANGA NA KARATU

Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki ya Exim Bw Stanley Kafu (Katikati) akikabidhi misaada ya vyakula na vinywaji kwa mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha New Faraja Orphanage kilichopo Mburahati jijini Dar es Salaam ili kuwawezesha watoto hao waweze kufurahia Sikukuu ya Eid-Ul-Fitr kama watoto wengine waliopo majumbani. Msaada wa aina hiyo pia ulitolewa na benki hiyo kwenye mikoa ya Mbeya, Shinyanga na Wilaya ya Karatu.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa benki ya Exim Bi Mariam Mwapinga (Katikati) akikabidhi misaada ya vyakula kwa mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha New Faraja Orphanage kilichopo Mburahati jijini Dar es Salaam ili kuwawezesha watoto hao waweze kufurahia Sikukuu ya Eid-Ul-Fitr kama watoto wengine waliopo majumbani.
Mlezi Mkuu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha New Faraja Orphanahe Centre  kilichopo Mburahati jijini Dar es Salaam Bi Zamda Idrissa (wa pili kulia) akitoa neno la shukrani kwa benki ya Exim kufuatia msaada huo. Wanaoshuhudia nipamoja na Diwani wa Kata ya Makurumla, wilayani Ubungo Bw Bakari Kimwanga (wa kwanza kulia)
Meneja Benki ya Exim tawi la Mbeya Bi Shamsa Shambe (Kushoto) akikabidhi misaada ya vyakula kwa mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Madina cha jijini Mbeya Bi Aisha Hamisi ili kuwawezesha watoto hao waweze kufurahia Sikukuu yaEid-Ul-Fitr kama watoto wengine waliopo majumbani
MenejaBenki ya Exim tawi la Mbeya Bi Shamsa Shambe (Kulia) akikabidhi msaada ya vyakula kwa mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Nuru cha jijini Mbeya Bi Mary Kassim ili kuwawezesha watoto hao waweze kufurahia Sikukuu yaEid-Ul-Fitr kama watoto wengine waliopo majumbani.
Baadhi ya wafanyakazi  benki ya Exim tawi la Mbeya wakiongozwa na Meneja wa tawi hilo Bi Shamsa Shambe (wa pili kulia) wakifurahia pamoja na watoto na uongozi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Nuru cha jijini Mbeya mara baada ya kukabidhi msaada wa chakula ili kuwawezesha watotohao waweze kufurahia Sikukuu ya Eid-Ul-Fitr kama watoto wengine waliopo majumbani.
Meneja Benki ya Exim tawi la Shinyanga Bi Sarah Tito (Kushoto) akikabidhi misaada ya vyakula kwenye kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum cha Buhangija kilichopo Mkoani Shinyanga ili kuwawezesha watoto hao waweze kufurahia Sikukuu ya Eid-Ul-Fitr kama watoto wengine waliopo majumbani.
Meneja Benki ya Exim tawi la Shinyanga Bi Sarah Tito (wa tatu kulia) akizungumza wakati akikabidhi msaada ya vyakula kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha Shinyanga Society for Orphans kilichopo Mkoani Shinyanga ili kuwawezesha watotohao waweze kufurahia Sikukuu ya Eid-Ul-Fitr kama watoto wengine waliopo majumbani.
Baadhi ya wafanyakazi  benki ya Exim tawi la Shinyanga wakiongozwa na Meneja wa tawi hilo Bi Sarah Tito (katikati) wakifurahia pamoja na watoto na uongozi wa kituo cha kulelea watoto yatima chaShinyanga Society for Orphans kilichopo Mkoani Shinyanga mara baada yakukabidhi msaada wa chakula ili kuwawezesha watoto hao waweze kufurahia Sikukuu ya Eid-Ul-Fitr kama watoto wengine waliopo majumbani.
Baadhi ya wafanyakazi  benki ya Exim tawi laKaratu wakiongozwa na Meneja wa tawi hilo Bw John Ndyebonera (katikati) wakifurahia pamoja na watoto na uongozi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Shalom Orphanage and Children  Care Centre cha Wilayani Karatu wakati  wakikabidhi msaada wa chakula ili kuwawezesha watoto hao waweze kufurahia Sikukuu ya Eid-Ul-Fitr kama watoto wengine waliopo majumbani.

 ****

Dar es Salaam: Mei 11,2021; Benki ya Eximimetoa msaada wa vyakula na vinywaji kwenye vituo vinne  vya kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingiramagumu vya jijini Dar es Salaam, Mbeya, Shinyanga na Karatu  ikilenga kuwawezesha watoto hao waweze  kusherehekea vizuri sikukuu ya Eid El Fitr.

Msaadahuo ulikabidhiwa na viongozi waandamizi wa benki hiyo wakiwa wameambatana nawafanyakazi wengine na ulihusisha mahitaji muhimu ikiwemo mchele, mafuta yakupikia, sukari, unga wa sembe, unga wa ngano, maharage pamoja na katoni zajuisi na maji ya kunywa.

JijiniDar es Salaam, akiwasilisha msaada huo katika kituo cha kulelea watoto yatimana wanaoishi katika mazingira magumu cha New Faraja Orphanage Centre  kilichopo Mburahati jijini humo, MenejaMasoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim Bw Stanley Kafu alisema imekuwa niutaratibu wa benki hiyo kusaidia makundi na taasisi mbalimbali kupitia ppangowake wa uwajibikaji kwa Jamii (CSR) unaofahamika kwa jina “Exim Cares”.

“…Msaadahuu ni maalum kwa ajili ya kusherehekea siku kuu ya Eid El Fitr, na ni mwendelezowa utaratibu wetu wa kile ambacho tumekuwa tukikifanya kila mwaka ambapowafanyakazi wa benki ya Exim pamoja na uongozi kwa ujumla tumekuwa tukiguswakuhakikisha kwamba watoto wanaoishi kwenye vituo hivi wanafurahia Sikukuu hizikama wenzao waliopo majumbani,'' alisema.

BwKafu alivitaja vituo vingine ambavyo vimekabidhiwa msaada huo ni pamoja naKituo cha Watoto Yatima cha Nuru kilichopo jijini Mbeya, Kituo cha ShinyangaSociety for Orphans na kituo cha watoto wenye mahitaji maalum cha Buhangija vilivyopomkoani Shinyanga pamoja na Kituo cha Shalom Orphanage and Children  Care Centre kilichopo wilayani Karatu.

ZaidiBw Kafu alitoa wito kwa watoto hao kuhakikisha wanasoma kwa bidii hukuwakitanguliza nidhamu kwenye kila jambo wanalofanya ikiwemo masomo na shughulizao za kila siku wawapo shuleni na kituoni hapo.

“Imekuwani furaha kwetu Benki ya Exim kuona kwamba tumekuwa tukipata wafanyakazi nawateja wenye mafanikio makubwa ambao baadhi yao wamepitia katika vituo hivi na kwasasawanafanya kazi zao kwa bidii na kwa weledi mkubwa. Ili hayo yatimie na kwenupia ni wajibu wenu kusoma kwa bidii pamoja na kutii maagizo ya walezi wenu kwanidhamu kubwa,’’ alisema.

Kwaupande wao wawakilishi wa vituo hivyo waliishukuru benki ya Exim kwa uamuziwake wa kuwakumbuka watoto yatima ili nao waweze kusherehekea vizuri siku kuuya Eid El Fitr kama ilivyo kwa familia nyingine majumbani huku wakiomba taasisihiyo na wadau wengine kuendelea kuwasaidia kutatua changamoto mbalimbalizinazowakabili.

“Tunashukurusana benki ya Exim na wafanyakazi wote kwa kuguswa na kuona umuhimu wakuesherekea siku hii muhimu na watoto yatima. Tunaomba waendelee kuguswa iliwatusaidie zaidi katika kutatua changamoto nyingine ikiwemo suala la bima zaafya kwa watoto kwa kuwa baadhi yao hawana bima hizo muhimu.'' alisema Bi ZamdaIdrissa Mlezi Mkuu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha New Faraja  kilichopo Mburahati jijini Dar es Salaam.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments