TAEC YAENDESHA MAFUNZO YA KITAIFA YA USAFIRISHAJI SALAMA WA VIFAA VYANZO VYA MIONZI


Mkuu wa kanda ya Mashariki ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) Dk.Wilbroad Muhogora akizungumza na waandishi wa Habari maara baada ya ufunguzi wa Mafunzo ya kitaifa ya utunzaji na usafirishajj salama wa vyanzo vyenye asili ya mionzi, mafunzo hayo yanahudhuriwa na washirki kutoka Taasisi mbali mbali zinazojihusisha na usafirishaji wa vyanzo vya mionzi nchini.Mkuu wa kanda ya Mashariki (TAEC) Dk Wilbroad Muhogora akifungua Mafunzo ya kitaifa ya utunzaji na usafirishajj salama wa vyanzo vyenye asili ya mionzi, mafunzo hayo yanahudhuriwa na washirki kutoka Taasisi mbali mbali zinazojihusisha na usafirishaji wa vyanzo vya mionzi nchini.
Picha ya pamoja na Washiriki

***


TUME ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), inaendesha mafunzo ya siku Tano (5) ya Kitaifa ya utunzaji na usafirishaji salama wa vyanzo vyenye viasili vya Mionzi (Radioactive source), kwa taasisi mbalimbali zinazojihusisha na usafirishaji wa mionzi nchini.


Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo yanayoendelea Jijini Dar es Salaam, Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), Dk. Wilbroad Muhogora, Mkuu wa Kanda ya Mashariki amesema kuwa mafunzo haya ni muhimu sana kwani yatawasiaidia washiriki kupata ujuzi wa kuhusu utunzaji na usafirishaji bora na salama wa vyanzo vya mionzi.

Dk Muhogora amesema lengo la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo katika menejimenti ya utunzaji na usafirishaji salama wa vyanzo vya mionzi.

"Usafirishaji wa vyanzo hivi unaweza kusababisha madhara iwapo matakwa ya kiulinzi na usalama hayatazingatiwa wakati wa kuvitunza au kuvisafirisha

Kwa hiyo mafunzo haya yatawasaidia kupata uelewa zaidi na kutayarisha mipango ya kinga mionzi wakati wote". Alisema Dkt. Muhogora.

Vifaa vyenye mionzi vinatumika nchini katika sekta mbali mbali za kijamii na kiuchumi ikiwemo afya, kilimo, ufugaji, viwanda, barabara ambapo mpaka sasa sasa jumla ya idadi ya vifaa vitoavyo mionzi nchini ni karibu 900 na kati ya hivyo vyanzo vya mionzi vyenye viasili vya mionzi (radioactive sources) ni 400.

Mafunzo haya yanahudhuriwa na washiriki kutoka katika taasisi mbali mbali zinazojihusisha na usafirishaji wa vyanzo vya mionzi nchini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments