AUAWA NA KUTUPWA MAKABURINI...VIJANA WAWILI WAUAWA KWA TUHUMA YA WIZI WA KUKU MWANZA

 Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza Linafanya Upelelezi Na  Ufuatiliaji Mkali Kufuatia Matukio Mawili Yaliyo  Tokea Kwa Nyakati Tofauti Katika Wilaya Ya  Nyamagana.



Tukio La Kwanza,
Tarehe 16.04.2021 Majira Ya 08:00 Hrs Katika Mtaa Wa Ipuli,  Kata Ya Mahina, Wilaya Ya Nyamagana, Ulikutwa Mwili Wa Mtu Mmoja Anayekadiriwa Kuwa Na Umri Wa Miaka 35, Akiwa Ameuawa Na Kutelekezwa Eneo La Makaburi. Jeshi  La Polisi Linaendelea Na Upelelezi Wa Kina Ili Kubaini  Wahusika Na Kuwakamata Na Kuwafikisha Maakamani Haraka Iwezekanavyo. Mwili Wa Marehemu Umehifadhiwa  Hospitali Ya Rufaa Bugando Kwa Uchunguzi Zaidi.

Tukio La Pili,
Tarehe 16.04.2021 Majira Ya 06:00hrs Huko Maeneo Ya Bukaga,  Kata Ya Kishiri, Wilaya Ya Nyamagana, Vijana Wawili Jinsi  Ya Kiume Ambao Bado Kufahamika Utambulisho Wao, Wanaokadiriwa Kuwa Na Miaka Kati Ya 18-23, Waliuawa Kwa Kushambuliwa Sehemu Mbalimbali Za Miili Yao Kwa  Kupigwa Mawe Na Kundi La Watu Ambao Baadae  Walitawanyika Na Kukimbia Waliwatuhumu Watu Hao  Kujihusisha Na Matukio Ya Wizi. Eneo La Tukio Kulikutwa  Kuku Watano Na Pikipiki Yenye Usajili Mc 607 Cpk Mali  Walizotuhumiwa Kuiba. Miili Ya Marehemu Imehifadhiwa  Hospitali Ya Rufaa Bugando Kwa Uchunguzi Na Utambuzi.  Msako Mkali Unaendelea Maeneo Yote Ilikukamata Wale  Wote Waliohusika Na Mauaji Hayo Kwa Kujichukulia Sheria  Mkononi.

Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza Linawataka Wananchi  Kuacha Vitendo Vya Kujichukulia Sheria Mkononi Kwani  Kufanya Hivyo Nikutenda Kosa La Jinai. Na Wale Wote  Waliohusika Kwa Mauaji Hayo Watakamatwa Na  Watafikishwa Mahakamani.

Imetolewa Na;
Muliro J. Muliro- Acp
Kamanda Wa Polisi (M) Mwanza.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments