MWANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE AFARIKI KWA KUPIGWA NA RADI

Mwanafunzi wa kidato cha nne  wa shule ya sekondari Kabugalo iliyopo Bukoba mkoani Kagera Gisera Oswardi (18) amefariki dunia  kwa kupigwa na radi huku mwalimu wake akijeruhiwa. 

Inaelezwa kuwa tukio hilo limetokea leo Alhamisi Aprili 15, 2021 saa tatu asubuhi ambapo mwanafunzi huyo akiwa na mwalimu wa shule hiyo Charles Alphonce walipigwa  na radi wakati wanatoka darasani kwenda ofisini.

Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kagera Dkt. Mselata Nyakiroto amesema uchunguzi wa awali umeonyesha kifo cha mwanafunzi huyo kimetokana na radi kumuunguza sehemu kubwa za mwili wake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments