MAWAZIRI WA WIZARA ZA VIWANDA NA BIASHARA, NA WIZARA YA UWEKEZAJI WAKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA MAREKANI NCHINI

 

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo akizungumza na wanahabari mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo na Balozi wa Marekani Bw. Donald Wright ambapo wamefanya mazungumzo kuhusu fulsa za uwekezaji hapa nchini.

Waziri wa Uwekezaji Mhe. Geoffrey Mwambe akizungumza na wanahabari mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo na Balozi wa Marekani Bw. Donald Wright ambapo wamefanya mazungumzo kuhusu fulsa za uwekezaji hapa nchini.

Balozi wa Marekani Bw. Donald Wright akizungumza wakati wa kikao na Mawawiri wawili wa Wizara mbili Viwanda na Biashara, na Uwekezaji walipokutana kujadili fulsa za uwekezaji hapa nchini.

Mawaziri na Naibu Waziri wakiwa katika mazungumzo na Balozi wa Marekani Bw Donald Wright walipokuwa wakizungumzia fursa za uwekezaji hapa nchini.

Balozi wa Marekani Bw Donald Wright akimkabidhi kitabu Waziri wa Uwekezaji kinachoonesha fursa mbalimbali zinazohitajika kuwekeza, mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao yaliyofanyika jana April 14,2021 jijini Dodoma,kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Prof.Kitila Mkumbo akionyesha kitabu hicho.

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo na Waziri wa Uwekezaji Geoffrey Mwambe wakipitia kitabu chenye fulsa za uwekezaji walivyokabidhiwa na Balozi wa Marekani Bw Donald Wright mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo.

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo watatu kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Uwekezaji Geoffrey Mwambe, na Balozi wa Marekani Bw. Donald Wright wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo kuhusu fulsa za uwekezaji.


Na.Alex Sonna,Dodoma

Mawaziri wawili wa Wizara za Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo na Wizara ya Uwekezaji Geoffrey Mwambe wamekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani hapa nchini Bw. Donald Wright kwa lengo la kujenga ushirikiano na kushirikishana fursa za uwekezaji zinazopatikana hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya mazungumzo hayo Waziri ya Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo amesema katika mazungumzo yao wamelenga kukuza biashara na uwekezaji baina ya nchi mbili za Tanzania na Marekani.

“Leo tumekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani hapa nchini Bw. Donald Wright, kuona namna ya kukuza ushirikiano wetu uliopo baina ya nchi hizi mbili, bado tunafursa nyingi na kubwa za wafanyabiashara wetu kutumia fursa hiyo” amesema Prof. Mkumbo.

Amesema katika mazungumzo hayo wamekubaliana kuweka jitihada za kuhakikisha nchi hizo mbili zinazidi kushirikiana katika nyanja za kiuwekezaji na kuleta manufaa na kuwawezesha wafanyabiashara kuwanya biashara kukuza uchumi wa nchi na mtu mmoja moja.

Amesema katika mazungumzo hayo pia wamezungumzia kuhusu mazao ya kimkakati hasa katika kuchakata na sio kuuza malighafi, na hatimaye mazao hayo yachakatwe hapa nchini na kuuza bidhaa badala ya kuuza malighafi, na sekta ya matunda ambayo yanapatikana kwa wingi hapa nchini.

Nae Waziri wa Uwekezaji Mhe. Geoffrey Mwambe amesema katika mazungumzo hayo pia wamezungumza kuhusu uwekezaji katika sekta mbalimbali ikiwamo ya afya hapa nchini, na wameonekana kuridhika na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika uwekezaji.

Amesema wawekezaji kutoka Marekani wameonyesha wapo tayari kuja kuwekeza hapa nchini ambapo tayari kuna kampuni imeonyesha nia ya kuja kuwekeza katika sekta ya mawasiliano kwa kuwekeza katika kampuni ya simu, na kampuni ya utalii kutoka Arusha imeonyesha nia ya kutaka kuongeza zaidi uwekezaji.

Ameongeza kuwa “Tumeongelea uchakataji wa mazao na ukiangalia Marekani ananunua korosho nchi flani, na ukiangalia sisi tunauza korosho ghafi na hizo nchi zinachakata na kuuza marekani, na sisi sasa tunaweza kuzichakata hapa nchini na kuuza Marekani” amesema Waziri Mwambe.

Amesema pia yapo mazao mengine ya kumkakati kama Kahawa na Pamba ambayo yatachakatwa na kuuzwa nje ya nchi hatimaye kama nchi kupata mapato kupitia kodi na kukuza ajira kwa wananchi ambao watapata ajira katika viwanda hivyo vitakavyoanzishwa.

Amesema katika mazungumzo hayo wamekubaliana kufanya majadiliano mara kwa mara ili kuuisha makubaliano yao ambapo watakuwa wakifanya tathmini kuona makubaliano hayo yanavyofanya kazi katika kuimarisha ushirikiano uliopo kwa miaka sitini sasa baina ya haya mataifa mawili.

Kwa upande wake Balozi wa marekani nchini Tanzania Mhe. Donald J. Wright amefurahishwa na ushirikiano wa kudumu wa Zaidi ya miaka 70 uliopo kati ya Tanzania na Marekani na

Mhe.Wright ameahidi kuwa Serikali ya Marekani itashirikiana kwa dhati na kwa karibu na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha wawekezaji kutoka marekani wanakuja kuwekeza nchini Tanzania kwani nchi hii ina fursa nyingi za uwekezaji pamoja na hali nzuri ya ulinzi na usalama. Balozi Mhe. Wright amesema kuwa Marekani imetengeneza historia kubwa katika kusaidia maendeleo ya Tanzania katika miradi ya kupambana na magonjwa, Ulinzi, elimu, miundombinu n.k ambapo hiyo imepelekea uhusiano kati ya Marekani na Tanzania kuimarika zaidi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments