COSOTA YAMTOZA FAINI YA MILIONI 5 MWIGIZAJI WA FILAMU KWA KUGHUSHI NYARAKA ZA UMILIKI

Kaimu Meneja  Idara ya Usajili na Ugawaji wa Mirabaha COSOTA Bw.Philemon Kilaka (katikati) akikemea tabia ya la kughushi nyaraka za umiliki unaofanya na baadhi ya wanatasnia ya filamu nchini kwa lengo la kujipatia fedha kinyume na taratibu za Hakimiliki leo Aprili 21, 2021  katika kikao cha usuluhishi kilichofanyika katika Ofisi za COSOTA Jijini Dar es Salaam kati ya Mwigizaji Sabrina Abdallah (kushoto) aliyeghulishi umiliki wa kazi Filamu ya ‘Mama Nongwa’ inayomilikiwa na Bw. Jotham  Ngulika (kulia) baada ya Sabrina kukiri kufanya kosa hilo kwa kupatiwa filamu hiyo na Mpiga picha wa kazi hiyo (Cameraman) kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za COSOTA Dar es Salaam.

Mwigizaji Sabrina Abdallah (kushoto) akikiri na kuomba msamaha kwa kosa  la kughushi nyaraka mbalimbali za umiliki wa Filamu ya ‘Mama Nongwa’ na kuisajili  COSOTA kama mmiliki  kinyume na sheria umiliki wa kazi Filamu ya ‘Mama Nongwa’ inayomilikiwa na Bw. Jotham  Ngulika (kushoto) kwa kusema filamu hiyo alipewa na Mpiga picha wa kazi hiyo (Cameraman), leo Aprili 21,2021 wakati wa kikao cha kupata suluhu ya mmiliki halali wa kazi hiyo baada ya kazi hiyo kuwasilishwa na watu wawili kufanyiwa usajili, kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za COSOTA Dar es Salaam, katikati Kaimu Meneja  Idara ya Usajili na Ugawaji wa Mirabaha COSOTA Bw.Philemon Kilaka

Mmiliki wa  Filamu ya ‘Mama Nongwa’  Bw. Jotham  Ngulika (kulia) akiishukuru COSOTA kwa kufanikisha kumpata kurudisha ummiliki wa kazi yake baada ya Sabrina Abdallah kukiri kosa la kughushi umiliki wa kazi hiyo na kuisajili kinyume na sheria  na kuomba msamaha leo Aprili 21,2021 wakati wa kikao cha kupata suluhu ya mmiliki halali wa kazi hiyo baada ya kazi hiyo kuwasilishwa na watu wawili kufanyiwa usajili, kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za COSOTA Dar es Salaam, katikati ni Kaimu Meneja  Idara ya Usajili na Ugawaji wa Mirabaha COSOTA Bw.Philemon Kilaka na kushoto ni ya Mwigizaji Sabrina Abdallah aliyeghushi kazi hiyo na kuisajili.

 




Na Anitha Jonas – COSOTA, Dar es Salaam

 

Taasisi ya Hakimiliki Tanzania yamtoza  faini ya shilingi milioni tano Mwigizaji wa Filamu kwa kughushi nyaraka mbalimbali za filamu isiyo ya kwake na kuisajili kama mmililiki halali.

 

Akizungumza katika kikao hicho cha kupata suluhu ya Mmiliki halali wa Filamu ya ‘Mama Nongwa’ iliyokuwa imesajiliwa COSOTA na Mwigizaji Sabrina Abdallah kwa kughushi umiliki na mikataba mbalimbali, Kaimu Meneja Idara ya Usajili na Ugawaji Mirabaha COSOTA Bw. Philemon Kilaka alisema kitendo alichokifanya mwigizaji huyo ni kosa kisheria na ni ukiukwaji wa Sheria mbalimbali za nchi ikiwepo Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki na Sheria ya Mwenendo wa makosa ya jinai.

 

Katika kikao hicho kilichofanyika leo Aprili 21,2021 Jijini   Dar es Salaam baada ya mmiliki wa Filamu hiyo Bw.Jotham Ngulika kufika kusajili kazi hiyo na kuonekana filamu hiyo ilikwisha sajiliwa na Mwigizaji huyo  kama mmiliki halali.

 

"Kitendo alichokifanya Sabrina cha kughushi nyaraka mbalimbali ikiwemo mkataba wa Muongozaji,(Director),Mkataba wa Mwandishi wa stori pamoja na Mkataba wa Mpiga picha huku akiwa anafahamu kuwa ni kosa,tunampa onyo kali pamoja na faini hiyo na akirudia kosa hili tunamfutia uanachama, hii ikawe fundisho kwa watu wengine wenye kufikiria kufanya hivi au wenye tabia

 kama hii,’’alisema Bw.Kilaka.

 

Kwa upande wa Mwigizaji huyo Sabrina Abdallah alikiri kufanya kosa hilo la kusajili filamu hiyo kwa kughushi mikataba mbalimbali kinyume na sheria, ambapo alieleza  kuwa  filamu hiyo alipewa na Mpiga picha wa kazi hiyo (Cameraman).

 

"Nakiri kweli nimefanya kosa la kughushi nyaraka mbalimbali kuhusu umiliki wa kazi hii hivyo naomba msamaha kwa mmiliki wa kazi hii na COSOTA kwa usumbufu niliyosababisha na ahidi kuwa balozi wa kukemea matumizi ya kazi usiyo na umiliki nayo bila ridhaa ya mmiliki,"alisema Sabrina. 

 

Halikadhalika nae Mmiliki wa Filamu hiyo Bw. Jotham Ngulika aliishukuru COSOTA kwa kufanikisha kurudisha umiliki wa kazi yake na kufanikisha kumpata mhusika aliyekuwa amesajili kazi hiyo kwa kughushi kinyume na utaratibu.

 

Wito wa COSOTA kwa wadau wa kazi za ubunifu  ni kuacha kuibiana kazi kwani hilo kosa kisheria na linahatarisha ukuaji wa kisekta .

 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments