ASKARI WALIOOMBA RUSHWA YA MIL. 100 WAFUKUZWA KAZI


Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha limewafukuza kazi askari wanne na kuwasimamisha kazi wakaguzi wawili wa polisi ambao wanatuhumiwa kuomba na kupokea rushwa ya shilingi milioni 100.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo, na kueleza kuwa tukio hilo la kuomba rushwa walilitekeleza Machi 19, 2021, maeneo ya Arumeru.

Aidha Kamanda Masejo ameongeza kuwa wakaguzi pamoja na askari hao watakabidhiwa kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), mkoani humo kwa ajili ya kuendelea na taratibu za kiuchunguzi.

Inadaiwa kuwa askari hao waliomba rushwa kwa Profesa Justine Maeda, ambaye amewahi kuwa mshauri wa uchumi wa Rais wa awamu ya kwanza, Hayati Julius Nyerere, baada ya kumpekua nyumbani kwake na kukuta vipande viwili vya meno ya Tembo kwenye mzinga wa Nyuki.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments