WAZIRI ATAKA WALIMU KUCHANGAMKIA FURSA


Waziri ataka waalimu kuchangamkia FURSA. Sekta ya benki imepiga hatua kubwa sana Nchini Tanzania kwenye miaka ya 2000. Umuhimu wa sekta hii ndio ulimpelekea Waziri Suleiman Jafo kuwataka walimu nchini Tanzania kuchangamkia FURSA ya mikopo na huduma ya benki yao ya Mwalimu Commercial Bank ambayo sasa inawawezesha kupata huduma kupitia matawi, ATM. Mwalimu Wakala na Mwalimu mobile popote Tanzania. Akizungumza wakati wa kuzindua huduma ya Mwalimu Visa Card Waziri Jafo alisema kwa waalimu ambao wanalenga kujikomboa kiuchumi ni vizuri wakatumia huduma za Mwalimu bank kwani sio tu inawapa mikopo nafuu lakini pia inawajali kabla ya ajira na baada ya ajira yaani wakistaafu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments