Tazama Picha : POLISI SHINYANGA WAKAMATA KONDOMU ZILIZOPIGWA MARUFUKU...MALI ZA WIZI, SILAHA NA WAHALIFU 231 | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, April 29, 2021

Tazama Picha : POLISI SHINYANGA WAKAMATA KONDOMU ZILIZOPIGWA MARUFUKU...MALI ZA WIZI, SILAHA NA WAHALIFU 231

  Malunde       Thursday, April 29, 2021
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha vifaa vya kupigia ramli chonganishi 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limefanya Operesheni maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu na kufanikiwa kukamata wahalifu 231 wanaojihusisha na unyang’anyi wa kutumia silaha, wakata mapanga na waganga wa jadi wanaojihusisha na upigaji ramli chonganishi ambazo ni chanzo na kichocheo cha mauaji ya imani za kishirikina.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Alhamisi Aprili 29,2021, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema Operesheni hiyo imefanyika kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021 ambapo jumla ya watuhumiwa 231 walikamatwa,kati yao wanawake ni 71 na wanaume 160.

“Watuhumiwa 169 kati ya 231 wamefikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria na watuhumiwa 62 waliobaki watafikishwa mahakamani baada ya upelelezo kukamilika”,ameeleza Kamanda Magiligimba.

“Katika Operesheni hiyo tulifanikiwa kukamata Bunduki 14 kati ya hizo gobore 13 na Shortgun moja ilitengenezwa kienyeji. Bangi kilogramu 65 na mashamba ya bangi ekari 6,madawa ya kulevya aina ya  Heroine gramu 300,mirungi kilogramu 3 na gramu 250”,ameeleza.

Amesema pia walikamata magari mawili yenye namba za usajili T.673 AYK Toyota Sprinter na T.377 DNA Toyota IST, pikipiki 19 aina ya  SANLG, mazao ya misitu mbao 711 na pombe ya Moshi lita 407 pamoja na mitambo mine ya kutengenezea pombe ya kienyeji (moshi).

Mali zingine zilizokamatwa ni boksi 30 za Kondomu zilizopigwa marufuku, TV 14, Radio Sabufa 6, Computer 3, magodoro 12, mabati 15, betri za magari 12, baiskeli,jiko la gesi, betri za pikipiki 6, betri za solar 7, simu 7,mafuta ya diesel lita 240,Engine Oil lita 120,vitenge pc 42 pamoja na magauni 15 ya vitenge, maturubai mawili ya magari makubwa, nondo 36 na mabomba matano ya maji.

Kamanda Magiligimba ameongeza kuwa Operesheni hiyo pia ilinasa bidhaa mbalimbali zilizokwisha muda wake na madawa mbalimbali,vifaa tiba, vifaa mbalimbali vya kufanyia uhalifu,noti bandia 7 kati ya hizo 6 ni za elfu 5, moja elfu 10, mifuko ya nailoni iliyopigwa marufuku 1200 na mawe yadhaniwayo kuwa na dhahabu kilogramu 2.

Amesema misako hiyo ni endelevu  ikiwa ni pamoja na kubaini mitandao yote ya kihalifu ili kukabiliana nayo huku akiwasisitiza wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwa jeshi la polisi na kwamba kamwe jeshi la polisi halitasita kuchukua hatua kali kwa mtu yeyote anayejihusisha na matukio ya uhalifu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu Operesheni Maalumu iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021 ambapo jumla ya watuhumiwa 231 walikamatwa,kati yao wanawake ni 71 na wanaume 160. Picha na Kadama Malunde 1 blog
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha bunduki zilizokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha bangi zilizokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha mabati yaliyokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha pikipiki zilizokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha baiskeli iliyokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha vifaa vya kupigia ramli chonganishi vilivyokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha vifaa vya kupigia ramli chonganishi vilivyokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha baiskeli iliyokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha moja ya TV zilizokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha bangi zilizokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha magodoro yaliyokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha moja ya jiko la gesi lililokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha pombe ya kienyeji/moshi iliyokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha vipodozi vilivyokwisha muda wake vilivyokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha vifaa vya kuzimia moto vilivyokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha mashine iliyokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha panga la kufanyia uhalifu lililokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha kahawa iliyokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Muonekano wa vipodozi vilivyokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Muonekano wa pombe za kienyeji na vifaa tiba vilivyokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Mali mbalimbali zilizokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Sehemu ya pikipiki zilizokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,202.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post