WEKUNDU WA MSIMBAZI WAWASILI BUKOBA KUKABILIANA NA WAKATA MIWA KAGERA SUGAR


Na Abdullatif Yunus, Michuzi TV.

KLABU ya Simba tayari imewasili Mkoani Kagera mapema leo Aprili 20,2021 kusaka alama Tatu dhidi ya wenyeji wao Wakata miwa wa Kagera Sugar, ambapo Timu hiyo imewasili ikiwa na Kikosi chake kamili.

Wakiongea katika Mkutano na waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Coffee Tree Hotel Walimu wa Timu zote mbili wameonesha morali ya kupata ushindi kwa Timu zao, huku kila mmoja akionesha kuheshimu mwenzake kimchezo.

Akizungumza kwa Upande wake Kocha wa Kikosi Cha Wakata miwa wa Kagera Francis Baraza amesema Timu yake ipo sawa licha ya kuwa na majeruhi wachache huku akimwaga sifa kwa wapinzani wao kwa kile alichokisema kuwa Simba ni miongoni mwa Timu kubwa Afrika hivyo atapambana kupata ushindi.

Naye nahodha wa Timu ya Wekundu wa Msimbazi Mohammed Hussein amekiri kuwa Timu yao imekuwa Ikipata wakati mgumu hasa wanapokutana na Kagera Sugar katika Uwanja wa Nyumbani, Hali ambayo husababisha kupata Matokeo kwa tabu Sana.

Timu ya Simba itafanya mazoezi Jioni hii katika Uwanja wa Kaitaba tayari kwa kujiandaa na Mchezo wao wa Jumatano hii.





CHANZO - MICHUZI BLOG




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments