RAIS SAMIA AAGIZA SAKATA LA MABANDO 'VIFURUSHI' LISHUGHULIKIWE


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
**
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameitaka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kushughulikia sakata la kupanda kwa gharama za vifurushi vya simu lililozua mjadala mzito kuanzia Aprili 2, 2021.

Rais Samia ametoa agizo hilo leo Jumanne Aprili 6, 2021 Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu na Wakuu wa taasisi na Idara mbalimbali aliowateua Aprili 4, 2021.

"Kuhusu suala la mabando kulizuka rapsharapsha juzi hapa, Wananchi wakapiga kelele mkalituliza, kalifanyieni kazi lisizuke namna ile mpo mnaangalia hawa watu wanakuja tu na mambo yao mpaka wananchi washtuke na nyie ndio mnashtuka, kakaeni na kampuni za simu. ",amesema Rais Samia.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments