WEZI WAIBA KENGELE YA KANISA YENYE KILO 500 | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, April 28, 2021

WEZI WAIBA KENGELE YA KANISA YENYE KILO 500

  Malunde       Wednesday, April 28, 2021
Watu wasiojulikana wameripotiwa kuiba kengele ya kanisa la Virgin Mary Orthodox lililoko eneo la Limuru kaunti ya Kiambu nchini Kenya ambapo tayari maafisa wa polisi wanaendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo. 

Kulingana na Katibu wa kanisa la Virgin Mary Ordhodox  James Warari alisema genge la wezi lilivamia kanisa hilo Alhamisi, Aprili 22,2021 na kuiba kengele hiyo ambayo inasemekana kuwa na uzito wa kilogramu 500. 

"Kisa hicho kilitokea Alhamisi Usiku, tuliamka asubuhi na tukagundua kwamba kengele hiyo haikuwepo. Mtu mmoja hawezi akabeba kengele hiyo kwa sababu ni nzito sana. Tunajua kulikuwa na watu kadhaa walishirikiana kubeba," Warari alisema. 

Warari alisema kengele hiyo ilikuwa imetengenezwa na shaba na ilikuwa ikitumiwa kuwakumbusha waumini saa za kuomba na pia kupanga ratiba ya kanisa hiyo.

Inasemekana kengele hiyo ilinunuliwa kutoka ng'ambo na Warari amemrai Mkenya yeyote ambaye atataka kuuziwa asiinunue bali awasiliane na wasimamizi wa kanisa hiyo.

 "Tungependa mtu yeyote ambaye ataiona kengele hiyo awasiliane nasi, nisingependa inunuliwe na mtu yeyote, naomba ipelekwe afisi yoyote ya chifu ilioko eneo la Limuru, kengele hiyo ulinunuliwa ng'ambo na hatuwezi ipata nyingine kama hiyo hapa Kenya," Wariru alisema.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post