Picha : KATAMBI AFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO SHINYANGA MJINI... MACHINJIO YA NDEMBEZI YAMVURUGA 'SITAKUBALI'


Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (CCM) akivuka mto wakati wa ziara yake Jimboni leo Jumatatu Aprili 5,2021.
***
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (CCM),amefanya ziara ya kukagua na kutembelea miradi ya maendeleo katika kata 8 za Manispaa ya Shinyanga zikiwemo shule, zahanati, madaraja na machinjio ya kisasa ya ng'ombe.

Katambi amefanya ziara hiyo iliyolenga kukagua, kutembelea miradi na kusikiliza kero za wananchi leo imefanyika Jumatatu Aprili 5,2021 akiwa ameambatana na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. David Nkulila na kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mjini ikiongozwa na Katibu wa CCM wilaya hiyo Agnes Bashemu.

Mhe. Katambi ametembelea zahanati ya kata ya Kizumbi pamoja na kukagua ujenzi wa zanahati ya Mwamagunguli iliyopo katika kata ya Kolandoto na kuchangia shilingi milioni moja ili kuongeza nguvu katika ujenzi huo ambao umekwama tangu mwaka 2010 na zahanati ya kata ya Chibe ambayo ujenzi wa jengo la maabara umekwama kwa kipindi kirefu likiwa limeishia katika hatua ya msingi tu.

Hali Kadhalika Katambi ametembelea na kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Negezi kata ya Mwawaza na shule ya msingi Ng’wihando kata ya Old Shinyanga ambao unaridhisha na kuwapongeza wananchi kwa kuchangia nguvu kazi na kutumia vyema fedha za mfuko wa Jimbo ambazo alichangia.

Pia amejionea hali ya jengo la vyumba vya madarasa ya shule ya Sekondari katika kata ya Lubaga yaliyotelekezwa kwa kipindi kirefu na kuzitaka mamlaka zinazohusika kuangalia njia nzuri ya kutumia madarasa hayo ambapo Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. David Nkulila amesema wana mpango wa kuifanya shule hiyo kuwa shule Shikizi kwa shule ya sekondari Mwasele ili majengo hayo yatumike wakati utaratibu wa kusajili shule ya sekondari Azimio ukiendelea.

Aidha Katambi amejionea jinsi barabara na daraja linalounganisha kijiji cha Uzogore na Bugwandege katika kata ya Ibadakuli ilivyokatika kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha usumbufu kwa wananchi wa eneo hilo wakiwemo watoto na akina na mama na kuahidi kuwasiliana na mamlaka zinazohusika ili kutatua changamoto ya daraja hilo ambayo inadaiwa kuwa ni ya muda mrefu.

Pia ametembelea ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini iliyopo katika kata ya Mwawaza na kuchangia shilingi 500,000/= kwa ajili ya ujenzi huo.

Ziara ya Katambi imetua pia katika Machinjio ya kisasa ya ng’ombe yaliyopo katika kata ya Ndembezi na kuonesha kutoridhishwa na ujenzi wa machinjio hayo yenye gharama ya Shilingi Bilioni 5.57 ulioanza mwaka 2018 ukitarajiwa kukamilika mwaka 2019 lakini mpaka leo hauoneshi dalili yoyote ya kuanza kufanya kazi, haufunguliwi na hauoneshi matumaini ya kufunguliwa.

“Ujenzi wa mradi huu wa machinjio hauoneshi dalili zozote utaanza kufanya kazi lini. Sikubaliani na hatua ya ujenzi wa mradi huu ambao umetumia fedha nyingi kiasi cha shilingi Bilioni 5.1 mpaka sasa na haujaanza kufanya kazi na kuna mapungufu mengi katika mradi huu, hali inayofanya wananchi wakose kazi na ajira”,amesema Katambi.

Katambi amesema kutokana na mradi huo wa machinjio kukwama kuna mambo lazima yachunguzwe ili kuondoa mashaka na hatua za kisheria "Lazima hatua zichukuliwe ili tujiridhishe kama fedha zimetumika kihalali tujue,sasa ni wakati wa kuchukua hatua".

“Haiwezekani viwanda vya Shinyanga kila vinapoanzishwa vinakwama, kile kiwanda cha Old Shinyanga kilishakwama. Najua viongozi wengi wakiwemo Mawaziri wamewahi kufika hapa na kuahidiwa kuwa kiwanda kitafunguliwa punde lakini hakifunguliwi….Maelezo ni haya haya hatua hazikuchuliwa,Mimi sitakubali kiwanda kukwama,hatuwezi kuwa tunaimba kila siku, hatua hazichukuliwi, jambo hili nalichukua nitalipeleka katika mamlaka zinazohusika na ni lazima hatua zichukuliwe kwa yeyote aliyesababisha mradi huu ukwame.Ni lazima tujue mbivu na mbichi kama mradi huu unafunguliwa au la. Na kama haufunguliwi tujue fedha zimeenda wapi”,ameongeza Katambi.

Hata hivyo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. David Nkulila amesema manispaa ya Shinyanga kupitia kamati ya fedha imeagiza kuitwa na kuhojiwa kwa Wakuu wa Idara wa Manispaa ya Shinyanga akiwemo aliyekuwa Afisa Mifugo wa Manispaa,Afisa Mipango,Mhandisi,Afisa Manunuzi,Mhandisi Mshauri, Contractor wa mradi Home Africa Investment ili waeleze kuhusu sababu za kukwama kwa mradi huo na Mkurugenzi wa Manispaa achukue hatua za kisheria.

Katambi ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kumuenzi aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuchapa kazi na kushiriki katika kutekeleza miradi ya maendeleo akieleza kuwa Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu ataendelea kusimamia na kutekeleza Ilani ya CCM kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi.

Naye Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Bi. Agnes Bashemu amewataka viongozi wa CCM kuwaunga mkono viongozi waliopo madarakani na kuhakikisha wanahamasisha wananchi kuchangia katika miradi ya maendeleo na jeshi la sungusungu kuachana na tabia ya kuwapiga faini ‘Kuwatulija’ wananchi wasiochangia maendeleo badala yake wawaelimishe na kuwahamasisha kuchangia miradi ya maendeleo.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (CCM) akivuka mto katika kata ya Ibadakuli katika Jimbo la Shinyanga Mjini wakati wa ziara yake leo Jumatatu Aprili 5,2021 ambapo amefika katika daraja linalounganisha kijiji cha Uzogore na Bugwandege ambalo limekatika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (CCM) akivuka mto katika kata ya Ibadakuli katika Jimbo la Shinyanga Mjini wakati wa ziara yake leo Jumatatu Aprili 5,2021 ambapo amefika katika daraja linalounganisha kijiji cha Uzogore na Bugwandege ambalo limekatika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha
Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (CCM) akivuka mto katika kata ya Ibadakuli Jimbo la Shinyanga Mjini wakati wa ziara yake leo Jumatatu Aprili 5,2021 ambapo amefika katika daraja linalounganisha kijiji cha Uzogore na Bugwandege ambalo limekatika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha
Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (CCM) akiwa katika barabara korofi inayounganisha kijiji cha Uzogore na Bugwandege ambayo imekatika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha
Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (CCM) akiwa katika barabara inayounganisha kijiji cha Uzogore na Bugwandege ambayo imekatika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha
Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (CCM) akiwa katika daraja linalounganisha kijiji cha Uzogore na Bugwandege ambalo limeelemewa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha
Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (CCM) akiwa katika daraja linalounganisha kijiji cha Uzogore na Bugwandege
Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (CCM) akiwa katika daraja linalounganisha kijiji cha Uzogore na Bugwandege ambalo limeelemewa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha
Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (CCM) akiwa  katika daraja linalounganisha kijiji cha Uzogore na Bugwandege
 Kushoto ni Mstahiki Meya wa Manispa ya Shinyanga , Mhe. David Nkulila akizungumza na wananchi katika daraja linalounganisha kijiji cha Uzogore na Bugwandege
Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (CCM) akizungumza na wananchi katika daraja linalounganisha kijiji cha Uzogore na Bugwandege
 Wananchi wakimsaidia mwendesha bodaboda kuvuka katika mto uliokata barabara inayounganisha kijiji cha Uzogore na Bugwandege katika kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga
Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (wa pili kulia) na msafara wake akiwasili katika Machinjio ya Kisasa ya ng'ombe yaliyopo katika kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya jengo la machinjio ya ng'ombe katika kata ya Ndembezi
Kushoto ni Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. David Nkulila akimuongoza Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (kulia) katika Machinjio ya kisasa yaliyopo Ndembezi katika Manispaa ya Shinyanga.
Kushoto ni Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. David Nkulila akielezea kuhusu machinjio ya kisasa yaliyopo Ndembezi. Katikati ni Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (kulia) , kulia ni Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu
Katikati ni Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. David Nkulila akimwelezea Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (kulia) kuhusu kukwama kwa Machinjio ya kisasa yaliyopo Ndembezi katika Manispaa ya Shinyanga.
Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (katikati) akielezea kusikitishwa kukwama kwa  Machinjio ya kisasa yaliyopo Ndembezi katika Manispaa ya Shinyanga.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. David Nkulila akimuonesha  Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (kulia) sehemu ya Machinjio ya kisasa yaliyopo Ndembezi katika Manispaa ya Shinyanga.
Katikati ni Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. David Nkulila akimwelezea Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kuhusu kukwama kwa ujenzi wa zahanati ya Mwamagunguli katika kata ya Kolandoto ulioanza mwaka 2010 ambapo kuna boma ambalo halijakamilika.
 
Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (kulia) akizungumza katika zahanati ya Mwamagunguli kata ya Kolandoto ambayo ujenzi wake umekwama tangu mwaka 2010
Muonekano wa jengo la zanahati ya Mwamagunguli kata ya Kolandoto ambalo ujenzi wake umekwama tangu mwaka 2010.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. David Nkulila na Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini wakiteta jambo katika zanahati ya Mwamagunguli kata ya Kolandoto.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. David Nkulila akielezea kuhusu kukwama kwa ujenzi wa shule ya sekondari ya  kata ya Lubaga ambapo kuna vyumba vya madarasa , vyoo lakini hakuna wanafunzi.
Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini akiingia katika choo cha shule ya sekondari ya kata ya Lubaga 'Azimio' ambacho hakitumiki
Muonekano wa jengo lenye vyumba vya madarasa yasiyotumika katika kata ya Lubaga
Diwani wa kata ya Chibe, Peter Kisandu (kushoto) akimwelezea Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (kulia) changamoto zilizopo katika zahanati ya Chibe ikiwemo ukosefu wa jengo la maabara na umeme ambapo Katambi alichangia shilingi 200,000/- kwa ajili ya kufanya wiring ili umeme uletwe.
Diwani wa kata ya Chibe, Peter Kisandu (katikati) akimuonesha na kumwelezea Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (kulia) eneo palipojengwa msingi kwa ajili la jengo la maabara katika zanahati ya Chibe.
 Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (kushoto) akizungumza katika zahanati ya Chibe ambapo alichangia shilingi 200,000/- kwa ajili ya kufanya wiring ili umeme uletwe.
Diwani wa kata ya Old Shinyanga, Enock Charles Lyeta akimwelezea Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (katikati) kuhusu ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya msingi Ng'wihando
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. David Nkulila akielezea kuhusu ukamilishaji wa maboma ya madarasa katika manispaa ya Shinyanga
Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini akipongeza viongozi wa kata na wananchi wa Old Shinyanga kujenga vyumba vya madarasa katika shule zilizopo katika kata hiyo ikiwemo Ng'wihando ambapo pia alichangia fedha kwa ajili ya ujenzi huo.
Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini akiangalia darasa katika shule ya msingi Negezi kata ya Mwawaza lililojengwa kwa nguvu za wananchi ambapo pia alichangia fedha kwa ajili ya ujenzi huo.
Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini akizungumza katika nyumba ya Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini ambapo amechangia kiasi cha shilingi 500,000/= kwa Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Dotto Joshua (kulia) ikiwa ni sehemu ya mchango wake katika ujenzi huo katika kata ya Mwawaza.
Muonekano wa nyumba ya katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini inayoendelea kujengwa katika kata ya Mwawaza.
Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini akizungumza katika zanahati ya Kizumbi kata ya Kizumbi.
Diwani wa kata ya Kizumbi Reuben Kitinya akizungumza katika zanahati ya Kizumbi
Sehemu ya wananchi na wanachama wa CCM kata ya Kizumbi.
Sehemu ya watoa huduma za afya katika zanahati ya Kizumbi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments