HARMONIZE KUWABURUZA MAHAKAMANI WANAOSAMBAZA ZINAZODAIWA KUWA PICHA NA VIDEO ZAKE ZA UTUPU | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, April 14, 2021

HARMONIZE KUWABURUZA MAHAKAMANI WANAOSAMBAZA ZINAZODAIWA KUWA PICHA NA VIDEO ZAKE ZA UTUPU

  Malunde       Wednesday, April 14, 2021

 

Kwa mara ya kwanza msanii Harmonize amevunja ukimya kwa yanayoendelea mitandaoni kwa kusema atawafikisha Mahakamani wote ambao wanadaiwa kuvujisha picha, video na sauti siziso na maadili kwa lengo la kumchafua na kumdhalilisha.


Harmonize ametoa taarifa hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo kwanza amekana tuhuma hizo kwa kusema sio yeye kwenye picha na video hizo, pili atawafikisha Mahakamani wote waliohusika.

"Taarifa kwa Umaa, video zilizotengenezwa na kusambazwa mtandaoni zikiwa zinaonyesha sura yangu na kuunganishwa na utupu wa mtu mwingine kisha kuunganishwa na sauti yangu kwa lengo la kunichafua kunidhalilisha na kuharibu brand ambayo nimeitengeneza kwa mabilioni ya shilingi

"Sitaki kujua aliyetengeneza ni nani au kaipataje ila ninachosema ni kwamba yeyote aliyehusika na hili suala linalolenga kunichafua na kunidhalilisha lazima watafikishwa mahakamani ili kukomesha chuki na tamaa zinazoathiri watu wasio kuwa na hatia,  watanili?

Chanzo- Eatv

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post