CWT YAAWEKA MSIMAMO WA KUPINGA UANZISHWAJI WA BODI YA KITAALUMA YA WALIMU

 

Na Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Chama cha walimu Tanzania[CWT] kimesema kitaendelea kupinga na kukataa  juu ya zoezi la uanzishwaji wa Bodi ya kitaaluma ya Walimu Tanzania kwani  bodi hiyo imelenga kumkandamiza Mwalimu badala ya kumsaidia.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo April,13,2021 Rais wa Chama cha Walimu Tanzania[CWT]Leah Ulaya amesema majukumu yaliyooneshwa kwenye bodi hiyo  yanafanana nay ale   yanayofanywa na Tume ya Utumishi wa walimu  [TSC]iliyopo sasa.

“Mnamo  mwaka 2019 ,CWT kilialikwa kutoa maoni kuhusu uanzishwaji  wa Bodi hiyo ,kimsingi sisi CWT,tuliikataa  kwa nguvu zote  baada ya kusoma sheria hiyo  tukajiridhisha pasi  na shaka  kwamba chombo hiki  kililenga kumgandamiza mwalimu  badala ya kumsaidia ,aidha majukumu yaliyo kwenye bodi hiyo yanafanana  na yale yanayofanywa na Tume ya utumishi wa walimu ”amesema.

Rais huyo wa CWT ameendelea kufafanua kuwa”Mnamo Tarehe 12 April,2021 CWT tulialikwa na katibu wa bunge  kukutana na kamati ndogo ya Bunge ya sheria juu  ya kanuni za uendeshaji  wa bodi hiyo ambayo msingi wake  ni sheria mama ambayo sisi CWT  tulikataa tangu mwanzo,katika kikao hicho  cha tarehe 12,April,2021 Chama cha Walimu Tanzania  kiliendelea na msimamo wake  wa usitishwaji wa chombo hiki  na kuimarisha utendaji kazi wa Tume ya Utumishi wa Walimu[TSC].

Aidha,Rais huyo wa CWT ametaja   sababu kadhaa za msimamo  kupinga uwepo wa bodi hiyo kuwa ni pamoja na gharama za bodi ambapo uendeshwaji  utategemea pesa ya mwalimu mfukoni   na ada ni elfu hamsini kwa mwaka  pamoja na kupunguza utitiri wa vyombo vinavyomsimamia mwalimu  .

 “Bodi hii tunaipinga kwa nguvu zote kwa sababu ,uendeshaji wa bodi hii utategemea pesa ya walimu mfukoni kwa ajili ya usajili,leseni na ada kwa mwaka ambayo si chini ya Tsh.50,000/=,gharama za kusikiliza mashauri,gharama za semina  ya kila mwaka ambayo ni lazima  kuhuisha leseni hiyo ,kushindwa kufanya hivyo mwalimu  atanyang’anywa leseni  na hivyo kupoteza sifa ya kufundisha na sababu nyinyine ya kuikataa bodi hii ni kupunguza utitiri wa vyombo vinavyomsimamia mwalimu na majukumu yakifanan”amesema.

Makamu wa Rais wa CWT Dinah Mathamani ameiomba serikali kuendelea  kuwamini na kuwatia moyo walimu.

“Walimu tunafanya kazi kwa bidii na ukiangalia ufaulu umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka kinachotakiwa ni serikali kuendelea kuamini walimu pamoja na kuwatia moyo “amesema.

Katibu mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania[CWT] Deus Seif amesema endapo bodi hiyo itapitishwa makato ya mwalimu kila mwezi itakuwa ni Tsh. 4200 huku Naibu katibu Mkuu CWT,Maganga Japhet Bodi ya kitaaluma ya Walimu Tanzania haina faida yoyote bali itadidimiza uchumi wa walimu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments