DK. MZEE : ACHENI KUTUMIA DAWA ZA KUTIBU MALARIA BILA KUFANYA VIPIMO

 

Mratibu wa Malaria Mkoa wa Shinyanga Dr. Daniel Mzee

                        Na Josephine Charles - Malunde1 blog

Jamii imeaswa kuacha kutumia dawa za Kutibu Ugonjwa wa Malaria pasipo kufanya Vipimo katika Vituo vya kutolea huduma za afya kwani kufanya hivyo kuna sababisha usugu wa magonjwa mbalimbali katika mwili wa Binadamu.

 Hayo yamesemwa leo Alhamisi Machi 11, 2021 na Mratibu wa Malaria Mkoa wa Shinyanga Dk. Daniel Mzee wakati akizungumza katika Kipindi cha Mambo Leo kinachorushwa na Radio Faraja  Fm 91.3 Shinyanga kila Jumatatu hadi Ijumaa.

Dk. Mzee amesema nyumba bora nayo inachangia kupunguza tatizo la Malaria akieleza kuwa pamoja na kwamba maisha ni magumu basi Jamii ijitahidi kutumia Chandarua chenye Dawa,kuweka wavu dirishani ili Mbu wasipite pamoja na kuzingatia usafi wa mazingira.

 Amesema Kauli mbiu ya malaria inasema “ZERO MALARIA INAANZA NA MIMI”  hivyo kila mwananchi anapaswa kudhibiti vyanzo vya uenezwaji wa Ugonjwa wa Malaria ikiwa ni pamoja na kufyeka nyasi,kufukia vidimbwi vya maji kando ya nyumba anayoishi.

 Kwa Upande wa Takwimu ya Ugonjwa wa Malaria nchini Tanzania Dk. Mzee amesema Tanzania ina kiwango cha asilimia 7.3% ya maambukizi ya Malaria wakati kwa Mkoa wa Shinyanga kiwango cha maambukizi ni asilimia 6.1%.

 Aidha ameainisha viwango vya maambukizi ya Ugonjwa huo kwenye Halmshauri sita(6) za Mkoa wa Shinyanga ambapo Halmshauri ya Ushetu ndiyo inayoongoza kwa kuwa na maambukizi ya asilimia 11.1%  ikifuatiwa na Halmashauri ya Shinyanga ambayo ina asilimia 6.9%, Msalala asilimia 6.2%, Manispaa ya Kahama  ni asilimia 3.7% , Manispaa ya Shinyanga ina asilimia 3.1 na Kishapu ina asilimia 2.9%.

Tazama picha hapa chini

Mratibu wa Malaria Mkoa wa Shinyanga Dr. Daniel Mzee

Watangazaji wa Kipindi cha Mambo Leo kinachorushwa na Radio Faraja fm 91.3 Shinyanga Josephine Charles na Elisha Shambiti wakiwa Studio na Mratibu wa Malaria Mkoa Dr. Daniel Mzee.

Watangazaji wa Kipindi cha Mambo Leo kinachorushwa na Radio Faraja fm 91.3 Shinyanga Josephine Charles na Elisha Shambiti wakiwa nje ya studio baada ya kipindi katika Picha ya Pamoja na Mratibu wa Malaria Mkoa wa Shinyanga Dr. Daniel Mzee na Dereva wake.


Watangazaji wa Kipindi cha Mambo Leo kinachorushwa na Radio Faraja fm 91.3 Shinyanga Josephine Charles na Elisha Shambiti wakiwa nje ya studio baada ya kipindi katika Picha ya Pamoja na Mratibu wa Malaria Mkoa wa Shinyanga Dr. Daniel Mzee na Dereva wake.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments