MOTO WATEKETEZA LA CHAAZ PUB, SINZA MORI DARLeo Ijumaa Machi 05, 2021 moto mkubwa ambao chanzo chake hakikufahamika mara moja, umeteketeza bar maarufu ya La Chaz Pub iliyopo eneo la Sinza Mori Manispaa ya Kinondoni, Dar es salaam.

Moto huo ulianza majira ya saa 9 alasiri uliteketeza eneo kubwa na bar hiyo kabla ya Jeshi la zimamoto na uokoaji kufika na kufanikiwa kuzima moto huo.

Akielezea chanzo cha moto Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji jijini Ilala, Ndg. Elimino Shang'a amesema chanzo cha moto huo bado hakijafahamika na wanaendelea na uchunguzi, kuhusu thamani ya vitu vilivyoungua, taarifa rasmi itatolewa baadae. Picha na SamTiger, MichuziTV


Sehemu ya La Chaaz Pub inavyoonekana sasa baada ya kuteketea kwa moto huo.
Askari Polisi wakiendelea kusimamia ulinzi eneo la tukio.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post