MCHINA AKAMATWA KWA KUWACHARAZA VIBOKO MADEREVA WAILI


Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linamshikilia raia wa China Xiao Yong (33) kwa tuhuma za kuwashambulia kwa kuwacharaza viboko madereva wawili kwa madai ya kutumia fedha walizopatiwa kupeleka wilayani Kyela kwenye mashine za mchezo wa kubahatisha.

Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Urlich Matei jana Jumanne Machi 30, amewataja walioshambuliwa kwa viboko na kusababishiwa maumivu makali kuwa ni Ramadhani Ulodi (27) na Omary Miraji 25).

Amesema awali jeshi lilipata taarifa kutoka katika mitandao ya kijamii zikionyesha raia wa Tanzania wakichalazwa viboko na ndipo walipanza kufuatilia na kubaini lilitokea katika Mtaa wa Meta, Kata ya Mabatini Jijini hapa.

“Tulianza ufuatiliaji na kubaini Watanzania hao ambao ni waajiriwa wa Kampuni ya Bonanza,”amesema.

Matei amesema polisi hawajafurahishwa na kitendo hicho na kuonya raia wa kigeni kuachana na tabia ya kujichukulia sheria mikononi kwa kuwapiga waajiriwa wao badala yake wawafikishe katika vyombo vya dola.

Amesema mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa katika kituo kikuu cha polisi na atafikishwa mahakamani uchunguzi wa kesi hiyo utakapokamilika.

CHANZO - GLOBAL PUBLISHERS

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments