MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ASEMA CHANGAMOTO YA KUKATIKA UMEME SASA IMEKWISHA | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, March 17, 2021

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ASEMA CHANGAMOTO YA KUKATIKA UMEME SASA IMEKWISHA

  Malunde       Wednesday, March 17, 2021


Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa, tatizo la kukatika umeme mara kwa mara ambalo lilijitokeza katika maeneo mbalimbali nchini siku za hivi karibuni limemalizika.
Akizungumza na wakazi wa wilaya ya Muheza mkoani Tanga ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo, Makamu wa Rais amesema kuwa tatizo hilo limemalizika baada ya mitambo iliyokuwa na hitilafu kufanyiwa matengenezo.

Amesema tayari amezungumza na Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani na amemuhakikishia kuwa umeme hautakatika tena.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan alilazimika kumpigia simu Dkt Kalemani baada ya wakazi wa wilaya ya Korogwe kulalamikia tatizo la kukatika umeme mara kwa mara.

Amefafanunua kuwa tatizo hilo la kukatika kwa umeme mara kwa mara lilijitokeza kutokana na mitambo ya kufua na kusambaza umeme kupata  hitilafu, na hivyo kulilazimu Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kufanya matengenezo.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post