BUNGE LAMTHIBITISHA DR MPANGO KUWA MAKAMU WA RAIS WA TANZANIA

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limemthibitisha Dr. Philip Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa 100%.

Wabunge 363 wote waliokuwepo bungeni jijini Dodoma leo Jumanne Machi 30, 2021 wamepiga kura za NDIO kumthibitisha Dkt. Philip Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania.

Dkt. Mpango amethibitishwa baada ya kupendekezwa na Rais Samia Suluhu Hassan na jina lake kusomwa bungeni mjini Dodoma na Spika Job Ndugai.

“Naomba kutangazia Bunge hili na nchi yetu kwa ujumla kwamba kura za hapana hakuna hata moja, kura zote 363 ni kura za ndiyo kwa hiyo amepata asilimia 100 ya kura zote”,amesema Ndugai.

Rais Samia Suluhu Hassan alimpendekeza Philip Mpango kuwa makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Jina hilo liliwasilishwa bungeni asubuhi ya leo Jumanne na mpambe wa Rais katika bahasha maalum.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post