MWENYEKITI WA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU MKOA WA SHINYANGA SAIDI MANKILIGO, WACHEZAJI TIMU YA STAND UNITED WAOMBOLEZA KIFO CHA MAGUFULI


Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoani Shinyanga bw. Saidi Mankiligo akisaini Kitabu cha Kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Machi 21,2021.

****
Wachezaji wa Timu ya Stend United ‘Chama la Wana wakiongozana na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoani Shinyanga bw. Saidi Mankiligo wamejitokeza katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga kutoa salamu za rambirambi na kusaini Kitabu cha Kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu wa mkoa wa Shinyanga Saidi Mankiligo ametumia fursa hiyo kukabidhi kadi za bima ya afya kwa wachezaji wote 32 na viongozi watano wa Stend United kwa lengo la kumuenzi hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwa mchango wake uliotukuka katika sekta ya michezo.

Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa miguu mkoani Shinyanga , Saidi Mankiligo amesema kifo cha Dk. magufuli kimegusa sana sekta ya michezo kwa kuwa alionekana mara kwa mara akizungumzia michezo na hata kushiriki katika mashindano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.

“Lakini pia kifo cha Dkt. Magufuli kimegusa wanamichezo wote nchini . Ili kumuenzi nimeamua kutoa kadi za bima ya afya kwa wachezaji wote 32 na viongozi watano wa timu ya Stend United kwa malengo ya kumuenzi Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi iliyotukuka ya kujenga vituo vya afya, zahanati na hospitali katika mikoa na wilaya zote nchini”,amesema Mankiligo.

Nao baadhi ya wachezaji wa timu hiyo ya Stend United wamesema msiba wa hayati Magufuli umewagusa mioyo yao kwa kiasi kikubwa kwani alikuwa Rais mzalendo,mpenda maendeleo katika sekta zote ikiwemo sekta ya michezo.

Aidha wachezaji hao wamewaomba viongozi waliobaki madarakani kumuenzi Magufuli kwa kuendeleza sekta ya michezo na kuhakikisha Tanzania inafanya vizuri katika mashindano ya kitaifa na kimataifa ili kufikia ndoto alizokuwa nazo Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoani Shinyanga bw. Saidi Mankiligo akizungumza baada ya kusaini Kitabu cha Kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Machi 21,2021.
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoani Shinyanga bw. Saidi Mankiligo ( wa pili kulia) akiwa na wachezaji wa Stand United baada ya kusaini Kitabu cha Kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Machi 21,2021.
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoani Shinyanga bw. Saidi Mankiligo akikabidhi kadi za bima ya afya kwa wachezaji wa Stand United baada ya kusaidini Kitabu cha Kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Machi 21,2021.
Mchezaji wa Timu ya Stend United ‘Chama la Wana akisaini Kitabu cha Kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.


UPDATES ZOTE

Pakua / Download App ya Malunde 1 blog Tuwe tunakutumia taarifa zote moja kwa moja kwenye simu yako bure kabisa 

Bofya <<HAPA>> Mara Moja Tu



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments