RAIS SAMIA AONGOZA VIONGOZI NA WANANCHI DODOMA KUPOKEA MWILI WA HAYATI MAGUFULI


Vilio, huzuni na machozi vilitawala kila kona ya Jiji la Dodoma baada ya mwili wa aliyekua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli aliyefariki Machi 17 mwaka huu kutua jijini Dodoma.

Mwili wa Dk Magufuli ulitua katika uwanja wa Ndege wa Dodoma majira ya saa 12:54 za jioni na kupokelewa na Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Wananchi wa Jiji la Dodoma ambao licha ya mwili wa Hayati Dk Magufuli kuchelewa kufika bado walizidi kujipanga barabarani bila kuchoka wakiimba nyimbo za mapambio.

Wingi wa wananchi waliojumuika kwenye barabara za jiji la Dodoma wakiimba 'Jeshi Jeshi Jeshi, Rais Rais Rais, Baba Baba Baba, Magu Magu Magu huku wengine wakilia ni uthibitisho tosha kwamba Dk Magufuli alikua kipenzi cha watanzania.

Wananchi wa Dodoma waliusindikiza mwili wa Dk Magufuli kutokea Uwanja wa Ndege kupitia mitaa ya Chako Ni Chako kuelekea Bunge hadi Ikulu Chamwino .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Viongozi na Wananchi wa JiJi la Dodoma kupokea Mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ulipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Dodoma leo Machi 21,2021. (Picha na Ikulu)





Pakua / Download App ya Malunde 1 blog Tuwe tunakutumia taarifa zote moja kwa moja kwenye simu yako bure kabisa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments