HIZI HAPA FAIDA ZA NYWELE ZAKO KATIKA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKO
Nywele zinatoa ulinzi dhidi ya majeraha wakati wa mtu amelewa na joto wakati wa baridi kali.

Nywele hujitokeza katika sehemu tofauti katika mwili wa mwanadamu , na faida zake hutegemea sehemu inazojitokeza mwilini kulingana na tafiti kadhaa.

Kwa mfano, nywele katika mwili wa mwanadamu hujitokeza kichwani, kwenye kidevu, katika nyusi na chini ya macho masikioni puani na katika sehemu za siri.

Mbali na katika mikono na miguuni , karibia mwili mzima wa mwanadamu umezibwa na nywele, lakini katika maeneo mingine nywele hizo huwa ndogo na hazionekani moja kwa moja na kwengine ni nyingi kulingana na jeni za mwanadamu, jinsia na kabila analotoka.

Siku hizi, nywele huendelea kuwa na umuhimu katika maisha ya mwanadamu kwa njia nyingi, ikiwemo kutoa mapato kwa wasusi kwasababu ya umuhimu wa nywele miongoni mwa wanawake.

Katika kila eneo duniani, nywele hutumika kupodoa na kutoa uhalisia, na urembo wa wanadamu.

Hii imewafanya wengi kujaribu kuzitumia kwa namna ambayo inatumbua lengo lake na taaluma kwa mfano kuna nyota wa michezo kama vile wacheza kandanda , waimbaji, waigizaji wa filamu na wengineo ambao hujulikana kwa mitindo yao ya kunyoa na kutengeneza nywele.

Nywele zinaweza kutumika kutofautisha kati ya wanaume na wanawake, vijana kwa wazee.

Nywele huonekana na wengine kama chanzo cha majivuno na urembo na kutokana na hilo, watu hutumia mitindo tofauti ya nywele ili kuonyesha wanakotoka na maadili yao.

Inagharimu fedha chungu nzima kurekebisha , kupata mafuta kubadili rangi na kadhalika. Siku hizi watu hutumia, mitindio ya ususi kubaini eneo mtu analotoka, dini, tabia na alivyolewa.

Lakini kitu muhimu zaidi ambacho nywele hutoa kwa mwili ni ulinzi unazowapatia binadamu kwa njia nyingi.

1. Nywele

Wataalam wengine wamefanya utafiti na kuchapisha data kuhusu umuhimu wa nywele za binadamu katika mwili ambao sio kila mtu anajua.

Wanaelezea kwamba nywele hutoa kinga kwa ngozi kutokana na tisho la mazingira, mbali na kupokea jumbe kwa haraka na kuzituma kupitia neva za ubongo wa mwanadamu mara tu kunapotokea hatari.

Kulingana na Dkt Mehmet Oz, Mkurugenzi mkuu wa Kituo cha matibabu cha mjini New York, Marekani mwili wa mwanadamu una nywele milioni tano.

Dkt. Woru Baba Goni, mkurugenzi mkuu wa chuo kikuu cha mafunzo ya hospitali kaskazini mashariki mwa Nigeria, aliambia BBC kwamba nywele ni muhimu katika kuwa na ngozi yenye afya na kulinda dhidi ya viini na magonjwa.

Aliongezea kwamba ngozi huwa na nywele kwasabbu zinasaidia kudhibiti viwango vya joto katika mwili wa mwanadamu wakati wa misimu ya baridi.

Nywele hulinda dhidi ya athari ya baridi katika Ngozi. Baridi hufika katika unywele ambao hutuma ujumbe kwamba mwandamu huyo anahisi baridi sana.

2. Nywele za kichwani

Nywele za kichwani hutoa kinga dhidi ya jeraha wakati mtu anapokuwa mlevi na joto katika baridi kali.

Nywele zilizopo kichwani ni nyingi kushinda zote zilizopo katika sehemu nyengine mwilini.

Na kama Dkt. Baba Goni alivyoambia BBC, viambatisho vya nywele hutoa kinga dhidi ya joto na baridi kwa kulipatia fuvu la kichwa hali ya hewa yenye joto wakati wa baridi, na pia kutoa kinga dhidi ya majeraha.

Alisema: "Ni kinga maalum kwa ngozi ya kichwa kutokana na kuumia moja kwa moja, na pia kupunguza ukali wa pigo au zote mbili, pamoja na joto na mvuke unaotolewa na mwanga wa jua ambao unaweza kuwa na madhara kwa mtoto."

3. Nywele za masikioni

Nywele zilizopo katika sikio la mwanadamu huzuia vumbi na maambukizo mengine kuingia mwilini ili kuzuia matatizo.

Nywele katika sikio la mtu hufanya kazi na ufizi unaokua katika sikio kuzuia uchafu wowote au chembe za vumbi kuingia kwenye mfereji wa sikio.

Vilevile nywele ndogo husaidia kuhisi na kudhibiti hisia za kibinadamu.

4. Nywele za puani

Nywele za puani zinazuia vumbi na viini vingine vinavyoweza kuingia

Nywele za puani ni muhimu katika kujilinda dhidi ya Vumbi na viini vingine katika njia ya pua.

Hewa inayoingia puani huwa na viini ambavyo jicho la kawaida haliwezi kuona.

Viini hivyo vinaweza kutumia njia ya pua na kuingia katika mapafu na katika maeneo mengine ya mwili wa mwanadamu hali ambayo inaweza kusababisha madhara makubwa.

Lengo la nywele zilizopo puani ni kuchuja vumbi kutoingia puani.

Dkt Goni aliambia BBC kwamba umuhimu wa nywele hizo ni kutoa ulinzi na kudhibiti unyevu uliopo katika hewa tunayopumua.

Nywele hizo huzuia vumbi kutobeba bakteria ambazo haziwezi kuonekana na macho ya mwanadamu kupitia njia ya pua hadi katika mapafu ama katika tumbo na kusababisha uharibifu.

5. Nyusi

Nyusi hulinda macho kutokana na mwanga mkali wa jua na vumbi au uchafu wowote.

Nyusi ni muhimu sana katika kuimarisha muonekana wa uso wa mwanadamu, mbali na kumlinda dhidi ya vumbi au bakteria kutoingia jichoni mara moja, wanasema wataalam.

Nywele hizo humsaidia mwanadamu kutokana na mwanga mwingi na unyevu. Nyusi pia huwa tayari kuhakikisha kuwa macho ni masafi.

''Huzuia maji ya mvua ama jasho kuingia machoni moja kwa moja ili mwanadamu aendelea kuona vizuri.''

6. Nywele za sehemu za siri

Hulinda ngozi dhidi ya presha ya sehemu za siri kusuguana kwa njia ambayo huenda ikasababisha uchungu na kuchubua ngozi.

Hali hiyo hutokea wakati wa tendo la ndoa hivyo basi nywele husaidia katika kulinda ngozi.

Watalaam pia wanasema kwamba husaidia katika kujilinda dhidi ya maambukizi kufikia uke.

Vilevile, wataalamu kama vile Dkt. Woru Baba Goni wanasema kwamba nywele za sehemu za siri za mwanamke husaidia katika kujilinda dhidi ya bakteria na magonjwa mengine.

''Hata iwapo nywele zilizopo katika sehemu za siri hazivutii, kuzikata mara kwa mara husadia katika usafi wa mwili kwa mujibu wa daktari Goni.

Huku baadhi ya watu wakiachilia nywele zao zimee, wengine huzipunguza kila zinapomea.

7. Masharubu
Masharubu yanazuia uso kutokana vitu vingine vyeusi ambavyo vinaweza kudhuru ngozi

Mustachi kama nywele nyengine za mwilini hutoa ulinzi dhidi ya mwanga mkali wa jua ambao husababisha saratani.

Mustachi uhitaji kusafishwa kutokana na athari za bakteria.

Wataalamu wanasema kwamba kuna umuhimu wa kusafisha mustachi.

Kama ilivyo muhimu katika dini , na kimatibabu na hata kitamaduni kusafisha mwili wa mwanadamu , ni muhimu vilevile kusafisha nywele, hususun zile ambazo zimejificha katika mwili.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post