" NENDA SHUJAA....NENDA BABA..NENDA JESHI " WANANCHI DODOMA WAKIMLILIA JPMNa Charles James, Michuzi Tv

NENDA SHUJAA! Ni maneno ambayo walikua wanayatamka wananchi wa Jiji la Dodoma waliojitokeza kwenye uwanja wa Jamhuri kumuaga aliyekua Rais Dk John Magufuli ambaye anaagwa leo kitaifa.

Mwili wa Dk Magufuli umeingia majira ya saa tano katika uwanja wa Jamhuri ambapo kila aliyekuwepo uwanjani hapa alisimama kumpa heshima kiongozi huyo mashuhuri aliyesifika kwa kusimamia nidhamu serikalini.

Wananchi waliojitokeza uwanjani hapa sambamba na viongozi mbalimbali wameshindwa kujizuia kumwaga machozi huku wengi wao wakiimba jina lake na kumtaka akapumzike kwa amani.

" Nenda shujaa nenda Baba, Nenda Jeshi! Hakuna tunalokudai umetupa Makao Makuu, umetupa hadhi ya Jiji umeibadilisha Dodoma hatuna tunachokudai, kazi kubwa uliyoifanya itaendelea kuonekana na kudumu kwenye maisha yetu," Ni baadhi ya maneno ya wananchi wa Jiji la Dodoma.

Mwili wa Dk Magufuli utaagwa na viongozi wakuu wa Nchi na Kimataifa leo jijini Dodoma ndani ya uwanja kisha utazungushwa mara tano kiwanjani hapa ili kuwapa fursa wananchi kumuaga na baadae utazungushwa katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Dodoma ili kila Mwananchi aweze kutoa heshima zakePakua / Download App ya Malunde 1 blog Tuwe tunakutumia taarifa zote moja kwa moja kwenye simu yako bure kabisa 

Bofya <<HAPA>> Mara Moja Tu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post