Picha : KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM LEO DAR KUFUATIA KIFO CHA MAGUFULI | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, March 20, 2021

Picha : KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM LEO DAR KUFUATIA KIFO CHA MAGUFULI

  Malunde       Saturday, March 20, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Ukumbi tayari kushiriki Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, kilichofanyika leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kimefanyika kwa dharura kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM na Rais Dk. John Magufuli kufariki dunia Machi 17, 2021. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete ambaye pia amehudhuria kikao hicho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi wakiwa katika Ukumbi tayari kushiriki Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, kilichofanyika leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kimefanyika kwa dharura kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM na Rais Dk. John Magufuli kufariki dunia Machi 17, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi wakipitia makabrasha kabla ya kuanza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, kilichofanyika leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kimefanyika kwa dharura kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM na Rais Dk. John Magufuli kufariki Dunia Machi 17, 2021.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibara Dk. Ali Mohamed Shein na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa wakiwasili ukumbini kwenye kikao hicho.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akitoa utangulizi wa kuanza kwa kikao hicho.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akitoa utangulizi wa kuanza kwa kikao hicho.
Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete akiwa kwenye kikao hicho. Wa pili ni Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume.
Mwenyekiti wa UWT gaudentia Kabaka akimsalimia Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mzee John Malecela ambaye pia alihudhuria kikao hicho.

Wajumbe wakiwa ukumbini kwenye kikao hicho. Mbele ni Katibu wa NEC Oganaizesheni Pereira Silima na kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole.
Wajumbe wakiwa Ukumbini kwenye kikao hicho. Baadhi yao Mbele ni Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda
Maafisa Waandamizi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Makao Makuu wakiwa kwenye kikao hicho. Kulia ni Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Itikadi na Uenezi Ndugu Mwansasu.
Wajumbe waakiwa Ukumbini kwenye kikao hicho. Baadhi yao Mbele -Kulia ni Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa na nyuma yake ni Spika wa Bunge Job Ndugai.
Wajumbe Dk. Jakaya Kikwete na Amani Abeid Karume wakipitia makabrasha wakati wa kikao hicho. Nyuma yao ni Dk. John Mndolwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Herry James akipitia makabrasha wakati wa kikao hicho
Wajumbe wakiendelea kufuatia mazungumzo mbalimbali kwenye kikao hicho.👇

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Makongoro Nyerere akifuatili katika makabrasha wakati wa kikao hicho.

 Picha zote na Bashir Nkoromo- CCM BlogUPDATES ZOTE

Pakua / Download App ya Malunde 1 blog Tuwe tunakutumia taarifa zote moja kwa moja kwenye simu yako bure kabisa 

Bofya <<HAPA>> Mara Moja Tu


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post