WAZIRI MKUU AZINDUA MWONGOZO WA UWEKEZAJI MKOANI SINGIDA

 

WAZIRI anayeshughulikia Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji Mkoani Singida kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi na katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Angelina Lutambi

 

WAZIRI anayeshughulikia Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji Mkoani Singida kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi na katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Angelina Lutambi
Kikundi cha Ngoma Asili cha Sarakasi wakitumbuiza wakati wa uzinduzi wa Mwongozo huo
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi mwenye kilemba cheupe akishiriki kucheza ngoma ya asilina wadau mbalimbali


WAZIRI wa Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo akikagua baadhi bidhaa zilizoletwa na wadau mbalimbali
Kwaya ya Chuo cha Utumishi Singida wakitumbuiza wakati wa tukio hilo


Na John Mapepele, Singida

Waziri kuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassimu Majaliwa  amezitaka  Mamlaka zote za Mikoa  kujipanga kikamilifu kutangaza fursa za uwekezaji zinapatikana kwenye  mikoa yao kwa kushirikiana Kituo cha  Taifa  cha Uwezekezaji  ili kuhakikisha kuwa fursa zote zilizoainishwa kwenye  miongozo ya  uwekezaji  zinapata wawekezaji makini ili kuongeza  mapato na ajira kwa wananchi

 Akisoma  hotuba  ya Mheshimiwa Waziri Mkuu kwenye  tukio la uzinduzi wa Mwongozo wa Fursa za Uwekezaji Mkoa wa Singida,   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amesema kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo  wa miaka  mitano(5) Serikali imedhamilia  kuimarisha  ustawi wa wananchi wake  kwa kuzalisha ajira  milioni nane na kukuza uchumi wake kwa asilimia nane  hivyo uwekezaji  makini unatakiwa ili kufanikisha azma hiyo.

Amesema  ili kuwapata wawekezaji makaini watendaji wote wa Serikali hawana budi kutoa taarifa sahihi za fursa zinazopatikana  katika maeneo yao na utaratibu wote wa namna ya  kuufuata ili kuweza kuwekeza.

“Ndugu zangu ni muhimu sana tubadilike  taarifa za uwekekezaji tunazozitoa ziwe  sahihi na ziwe zinafanana, ukienda kwa Mkuu wa  Mkoa upate taarifa sawa na ukichukua taarifa hiyo kwa  Katibu Tawala wa Mkoa na Mkurugenzi Mtendaji wa  Halmashauri hapo tutakuwa tumefanikiwa” amesisitiza Profesa Mkumbo.

Amezitaka  mamlaka hizo kutowakwamisha  wawekezaji kwa  kuhakikisha  maeneo ya uwekezaji  yanapatikana mara moja ili pindi Wawekezaji wanapofika wanapatiwa   maeneo hayo na wanahudumiwa  kikamilifu ikiwa ni pamoja na kuondoa changamoto zozote zinazojitokeza.

Amesema  balozi  namba moja  anayeweza kuleta au kutoleta wawekezazi katika nchi yoyote  duniani ni Muwekezaji aliye ndani ya nchi husika  hivyo  ni muhimu  kuwapa huduma  bora  ili waweze kutuletea wawekezaji wengi zaidi ambapo amesisitiza  uwekezaji ufanywe kwa kuzingatia sheria, taratibu na miongozo ya  Serikali ili nchi yetu iweze kunufaika.

Amekemea tabia  ya kupenda kutoa lawama  baada ya  kuingia mikataba  mibovu na wawekezaji na badala yake amewataka  watendaji kuwa makini katika  mchakato mzima wa majadiliano na kufunga mikataba hiyo na wawekezaji.

Aidha, ameitaka  kila Mkoa kuangalia kuangalia maeneo  machache ya kipekee ili kufanya uwekezaji  wenye tija badala ya kwenda na maeneo mengi ambayo  hayana  tija.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kwa kubuni mikkakati  kabambe ya uwekezaji ambayotayari katika kipindi kifupi imeleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi na kijamii kwenye nchi yetu.

Amesema Mkoa wa Singida ni miongoni mwa mikoa ambayo ilikuwa ikionekana kama  mikoa masikini lakini sasa  umekuwa  ni miongoni mwa mikoa ambayo inaweza kuongoza  kuleta  mapato makubwa kwa nchi  kutokana na  kuboreshwa kwa  mazingira na fursa nyingi zilizopo.

Ametaja baadhi ya fursa za uwekezaji  zinazopatikana kuwa ni pamoja na madini, kilimo  cha Alizeti na Korosho, mafuta asilina na gesi pia elimu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post