JESHI LA POLISI LAMUACHIA ASKOFU MWAMAKULAAskofu Emmaus Mwamakula wa Kanisa la Uamsho la Moravian

 Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemuachia kwa dhamana Askofu Emmaus Mwamakula wa kanisa la Uamsho la Moravian baada ya kufanya upekuzi nyumbani kwake.

Akizungumza  leo Jumanne Februari 16,2021 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema baada ya jeshi hilo kwenda kufanya upekuzi nyumbani kwake limemuachia baada ya kutimiza masharti ya dhamana.

“Tumempuuza na baada ya kwenda kufanya upekuzi nyumbani kwake, mchana huu tumemuachia kwa dhamana baada ya kutimiza masharti,” amesema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post