JAMII YATAKIWA KULINDA BWAWA LA NYUMBA YA MUNGU

 

Makamu Mwenyekiti wa bodi ya Wakurungenzi ya Shirika la Umeme nchini TANESCO  Balozi James Nzagi akizungumza mara baada ya ziara yake ya kukagua kituo cha kuzalisha umeme cha bwawa la nyumba ya Mungu kilichopo mkoani Kilimanjaro.

MENEJA wa Pangani Hydro System Steven Mahenda akisisitiza jambo kwa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO) wakati wa ziara hiyo wa pili kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa bodi ya Wakurungenzi ya Shirika la Umeme nchini TANESCO  Balozi James Nzagi
Kaimu Mkuu wa kituo cha kuzalisha umeme cha Nyumba ya Mungu Mhandisi Edmund Seif kulia akisistiza jambo kwa Bodi ya Wakurugeni ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO) wakati wa ziara yao
Kaimu Mkuu wa kituo cha kuzalisha umeme cha Nyumba ya Mungu Mhandisi Edmund Seif kushoto akisistiza jambo kwa Bodi ya Wakurugeni ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO) wakati wa ziara yao
Kaimu Mkuu wa kituo cha kuzalisha umeme cha Nyumba ya Mungu Mhandisi Edmund Seif kushoto akisistiza jambo kwa Bodi ya Wakurugeni ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO) wakati wa ziara yao


Bwawa la Nyumba ya Mungu kama linavyo onekana kilichopo mkoani 
 
JAMII zinazoishi kando kando ya bwawa la Nyumba ya Mungu wameshauri kuacha shughuli zitakazochangia kuharibu bwawa hilo bali  walinde na kutunza chanzo hicho  ili kujihakikishia uzalishaji wa uhakika wa nishati ya umeme hapa nchini.

Ushauri huo umetolewa na Makamu Mwenyekiti wa bodi ya Wakurungenzi ya Shirika la Umeme nchini TANESCO  Balozi James Nzagi wakati wa ziara yake ya kukagua kituo cha kuzalisha umeme cha bwawa la nyumba ya Mungu kilichopo mkoani Kilimanjaro.

Alisema kuwa maji ndio nishati inayotumika katika kuendeshea mashine za kuzalisha umeme hivyo ipo haja ya jamii kuendelea kuelimishwa kulinda na kutunza vyanzo vya maji ili kujihakikishia uzalishaji wa uhakika wa umeme lakini na kwa ajili ya maendeleo yao.

"Jamii inatakiwa kukwepa kufanya shughuli ambazo zinahataridha uhai wa  maji ya bwawa la mto wa Nyumba ya Mungu kwani maji hayo  sio tuu yanatumiwa  na TANESCO bali hata wananchi wanategemea raslimali hiyo kwa matumizi yao " alisitiza Makamu Mwenyekiti huyo.

Hata hivyo aliwataka watumishi wa shirika hilo kuendelea kufanyakazi kwa uwadilifi ikiwemo kujiepusha na vitendo ambavyo vitasababisha kushusha hadhi yao na shirika kwa ujumla.

Vile vile alisema kuwa licha ya kuwepo kwa mitambo mikongwe ya kuzalishia umeme katiks baadhi ys vituo lakini ameweza kuridhishwa na namna inavyofanyakazi kwa ufanisi kama mitambo ya kisasa.

"Hiki nikichojionea ndio ile kauli ya Wahenga kwamba kitunze kidumu kwani uimara wa mitambo hii inatokana na marekebisho yanayofanywa mara kwa mara hii yote ni katika kuwahakikishia huduma bora watanzania" alisema Balozi Nzagi.

Kwa upande wake Meneja Mwandamizi Uzalishaji TANESCO makao makuu Steven Manda alisema kuwa shirika hilo lipo kwenye maboresho ya mitambo yako kutoka analogi kwenda kwenye digitali ili kuboresha utendaji wao wa kazi wa kutoa hudums bora.

"Maboresho hayo sasa yataweza kumaliza changamoto ya kukatika kwa umeme kwani kama kuna hitilafu mitambo itakuwa inataarifa mapema na hivyo hatua za marekebisho zinachukuliwa kwa haraka" alisema Manda.

Nae Kaimu Mkuu wa kituo cha kuzalisha umeme cha Nyumba ya Mungu Mhandisi Edmund Seif alisema kuwa kituo hicho kinazalisha umeme megawati 8 kwa kutumia mashine mbili.

Hata hivyo alisema kutokana na uwepo wa maji ya kutosha katika bwawa hilo kwa kipindi cha miaka mitatu mfululuzi hawajawahi kuzalisha chini ya kiwango.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post