TMDA KANDA YA ZIWA IMEKUWA NA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA UCHUNGUZI NA UTAFITI WA KIMAABARA

 
Kaimu Mkuu wa maabara ya TMDA Kanda ya Ziwa Bugusu Nywamweri akifafanua jambo kwa wanahabari.
Kaimu Mkuu wa maabara ya TMDA Kanda ya Ziwa Bugusu Nywamweri akiwa na baadhi ya wanahabari katika maabara hiyo.
Mtaalam wa Uchunguzi katika Maabara hiyo Kapiliya Lameck akiwa kazini.
Jengo la Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA Kanda ya Ziwa lililoko Bururuga Mwanza.

                                                        ............

Maabara ya TMDA, Kanda ya Ziwa ilianzishwa mwaka 2018 kwa lengo la kutoa huduma katika maeneo makuu mawili, upande wa Maicrobiolojia na upande wa Kemia.

Maabara hiyo imefanya uchunguzi wa dawa katika kipindi chote hadi sasa na uchunguzi huo wa kimaabara umekuwa na mafanikio makubwa.

Hayo yanaelezwa na Kaimu Mkuu wa maabara ya TMDA Kanda ya Ziwa Bugusu Nywamweri wakati akizungumza na wanahabari waliotembelea maabara hiyo hivi karibuni ili kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa katika maabara hiyo

Nyamweri anasema maabara hiyo ipo mahususi kwa ajili ya uchunguzi wa aina mbalimbali za vipukusi  hapa tuna mitambo ya kisasa ambayo inawezesha kufanya uchunguzi wa aina mbalimbali za sampuli kutoka maeneo mengi ya kiutafiti.

"Maabara hii imesheheni mashine za kisasa  na ina jumla ya watumishi sita ambapo kwa upande wa Microbiolojia wapo wawili na upande wa kemia wapo wanne" Anasema Nyamweri.

Kuna mitambo ya kisasa kama Liquid Cromatography Mass (LCMSMS),High Performance Liquid Chromatragraphy(HPLC) na pia kuna Microwave Plasma Atomic Emission Spectroscopy (MPAES)". 

Mashine hizo zimewekwa kwa gharama ya takribani Shilingi  bilioni tatu ambao ni uwekezaji mkubwa katika maabara hii na taasisi yenyewe.

Anaongeza kuwa "Ili  kupata bidhaa bora hasa za Dawa,Chakula,Vifaa tiba na vitendanishi ni muhimu kuwa na maabara zenye viwango na uwezo wa kufanya vipimo hivyo kwa ufanisi.

Mamlaka ya dawa, vifaa tiba (TMDA) ina nafasi kubwa katika kuhakikisha ubora ,usalama na ufanisi wa bidhaa kabla ya kutumika.

Ndiyo maana maabara kama hii ya TMDA ni  muhimu  katika kufanya vipimo,tafiti na majaribio mbalimbali ikiwemo ya dawa mbalimbali zinazozalishwa na kutumiwa na walaji.

Nyamweri anasema Maabara hiyo imekuwa ikifanya uchunguzi wa dawa mbalimbali ambapo kwa kipindi cha miaka mitatu tumeweza kupima jumla ya sampuli 860,”anabainisha.

"Tumefanikiwa pia kug’amua baadhi ya dawa ambazo zilikuwa na matatizo katika viwango au kuathiriwa na namna zinavyohifadhiwa hivyo kusaidia viwanda husika kufanya marekebisho". Anaongeza Nyamweri

Nywamweri anasema katika uchunguzi kuna wateja wa aina mbili ambao ni wateja wa ndani ikijumuisha wakaguzi wa mamlaka na wateja wa nje ambao ni wenye viwanda au watengenezaji wa bidhaa.

“Sampuli zinavyoletwa zinapokelewa kwa utaratibu katika mfumo wa kielektroni, tuna mfumo unaoitwa Lims Labatri Information Management System, zitapokelewa na wataalama na kisha kuingizwa kwenye mfumo na kutunzwa stoo kama zitakuwa zimekidhi vigezo vinavyotakiwa ili ziweze kufanyiwa uchunguzi.

“Zinapohitaji kuchunguzwa mtaalamu wa uchunguzi atachukua sampuli na kuzipeleka maabara kwa ajili ya uchunguzi na zoezi la uchunguzi linapokamilika mtaalamu husika atachukua majibu na kuingiza katika mfumo wa kielektroniki na kisha kuhakikiwa na mchunguzi mwingine mwenye utaalamu sawa au zaidi yake kwa ajili ya kujiridhisha kama taratibu zote za kiuchunguzi zimefuatwa.

Anasema baada ya kukamilika kwa uhakiki endapo hakutakuwa na tatizo katika mfumo wa majibu yatawasilishwa kwa msimamizi wa maabara au mkurugenzi kwa ajili ya kuhakiki na kutoa kibali cha kuandaliwa cheti cha majibu ya uchunguzi kupelekwa kwa muhusika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post