STAMICO YAPATA TUZO YA MCHANGIAJI BORA WA GAWIO SERIKALINIShirika la Madini la Taifa (STAMICO) imepata tuzo ya uchangiaji bora wa Gawio Serikalini katika sekta ya madini. Tuzo hii imetolewa na Wizara ya Madini katika mkutano unaondelea katika jijini Dar es salaam.

Akiongea mara baada ya kupokea tuzo hiyo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt Venance Mwasse amesema amefurahi kupata tuzo hiyo kwa kuwa ni sehemu ya kutambua na kuthamini michango wa Shirika kwa niaba wa Watanzania.
Amesema STAMICO itaendelea kutoa Gawio Serikalini kwa kuwa Shirika limejizatiti katika kuhakikisha sekta ya madini inawanufaishana Watanzania wote.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post