BABU ANAYEONGEA NA NYOKA AZUA GUMZO | MALUNDE 1 BLOG

Monday, February 1, 2021

BABU ANAYEONGEA NA NYOKA AZUA GUMZO

  Malunde       Monday, February 1, 2021


Mshereheshaji wa nyoka mwenye miaka 71, kutoka Nigeria aliyetambuliwa kama Audu amewachangamsha wanamtamdao na ujuzi wake wa kusemezana/kuongea na nyoka na kuwafanya kufuata amri yake.

Audu alisema wazazi wake pia walikuwa washereheshaji wa nyoka na alijifunza ujuzi huo kutoka kwao.

Katika video ambayo ilichapishwa kwenye kitandazi cha Twitter na @MobilePunch, Mshereheshaji huyo anaonyeshwa akiwaamuru nyoka kudensi na kweli walifuata amri yake.

Audu pa alikuwa akiwashindilia nyoka hao mdomoni mwake lakini wanyama hao hawakumdhuru.

Akizungumzia kuhusu ujuzi wake, Audu wazazi wake pia walikuwa washereheshaji wa nyoka alianza kusemezana na nyoka hao akiwa mvulana wa miaka saba.

 Alisema amejaaliwa watoto 10 na wote wanaogopa nyoka kando na mmoja ambaye anajifunza kusherehesha wanyama hao.

 Kulingana na Audu, nyoka wale hula nyama freshi na huwapeleka katika vituo tofauti jijini Lagos kutumbuiza.

Alisema nyoka hawapendi jua, na kuongezea kuwa hukereka sana wakianikwa kwenye jua. Audu alisema moja wa nyoka wake aliwahi kumuuma lakini alitumia dawa ya baba yake kujitibu.

 Donald Agbaje alisema: "Tunalipa pesa nyingi kumtazama mtu wa nyoka kwenye televsheni ilihali hapa tuna baba, ambaye amechaguliwa na ulimwengu wa kiroho na nguzu za kudhibiti kunyoka na kufuata amri yake."

 "Nimekuwa nikimfahamu huyu baba kwa miaka 18, jina lake ni Audu Alejo (Audu d sneak)...alikuwa akifanya miujiza na nyoka wake kwenye Mile12 kati kati ya watu wa Hausa/Yoruba ," Adebare Irenimoyan alisema.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post