TFF YAMTAMBULISHA KIM POULSEN KUWA KOCHA MPYA WA TAIFA STARS

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limemtambulisha Mdenmark Kim Polusen kuwa kocha mpya wa timu ya Taifa (Taifa Stars).

Kocha huyo amesaini mkataba wa miaka mitatu kuifundisha timu hiyo, ambayo hivi sasa iko katika mbio za kutafuta nafasi ya kucheza Fainali za AFCON pamoja na Kombe la Dunia ambazo zote zitafanyika mwaka 2022 katika nchi za Cameroon na Qatar.

Poulsen aliwahi kuifundisha Taifa Stars kati ya mwaka 2012 na 2013 ambapo kabla ya kupewa nafasi hiyo alikuwa kocha wa timu za taifa za vijana.

Kocha huyo anachukua nafasi ya Etienne Ndayiragije ambaye hivi karibuni alifikia makubaliano na TFF kuvunja mkataba wake. Ndayiragije aliteuliwa kuifundisha timu hiyo mwezi Julai mwaka 2019.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post