ALIYEPIGA MKE WAKE KWA MWIKO WA UGALI ATUPWA JELA DAR

Na Pamela Chilongola - Dar es salaam
Mahakama ya Mwanzo ya Buguruni imemhukumu kifungo cha nje cha miezi minne mkazi wa Tabata Segerea, Baraka Athuman (33) baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga mke wake Kuluthum Khamis kwa kutumia mwiko wa ugali kutokana na wivu wa mapenzi.

Pia, mahakama hiyo imemwamuru mshtakiwa amlipe mkewe huyo kiasi cha Sh20,000 kama fidia ya matibabu

Akitoa hukumu hiyo juzi Hakimu, Gladness Njau alisema ushahidi uliotolewa na mlalamikaji pamoja na mume wake Athumani kukiri mahakamani hapo kumpiga Kurutum sehemu mbalimbali ya mwili wake, ulitosha kumtia hatiani. Alidaiwa kumpiga kwa mwiko wa ugali baada ya kumfumania akiishi na mwanaume mwingine.

Alisema kupitia ushahidi uliotolewa na upande wa mlalamikaji pamoja na mshtakiwa mwenyewe mahakama hiyo imejiridhisha kuwa ni kweli alimpiga Kurutum sehemu mbalimbali ya mwili wake na kumsababishia maumivu makali mahakama hiyo inamtia hatiani.

Via Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post