RAIS MAGUFULI : NINATEGEMEA KUVUNJA HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, February 24, 2021

RAIS MAGUFULI : NINATEGEMEA KUVUNJA HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM

  Malunde       Wednesday, February 24, 2021

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amesema Serikali ina mpango wa kuvunja halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na kuchagua manispaa moja katika jiji hilo itakayopandishwa hadi na kuwa Jiji lengo likiwa kupunguza gharama zisizokuwa za lazima.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Jumatano Februari 24, 2021 wakati akizindua Daraja la Juu katika Makutano ya Barabara za Ubungo (Kijazi Interchange) Ubungo jijini Dar es Salaam.

“Ninategemea kuvunja Jiji la Dar es Salaam ili tutengeneze jiji la eneo fulani tunaweza kuifanya Ilala ndio iwe jiji itategemea na namna mambo yatakavyokwenda lakini kuwa na madiwani ambao wanakaa hapa juu wanachangiwa fedha na hawana miradi ya maendeleo hili nitalikataa”,amesema.

"Tunataka Manispaa moja katika jiji la Dar es Salaam ndio ipandishwe hadhi iwe jiji halafu nyingine ziwe manispaa. Jiji la Dar es Salaam litaendelea kuwepo lakini tutachukua eneo fulani na ninafikiri Ilala inafaa kuwa jiji maana ndio ipo katikati, Ubungo itasubiri maana barabara bado hazijatengenezwa,” amesema Rais Magufuli.

Amewataka viongozi ambao walijiandaa kuwa mameya wa jiji wajue hilo limekwisha.

Soma pia :
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post