KAMPUNI YA AKO GROUP LTD YACHANGIA VIFAA VYA UJENZI WA MADARASA NA OFISI YA WALIMU SHULE YA MSINGI KABALE -KAKOLA

Makabidhiano ya mifuko ya saruji iliyotolewa na Kampuni ya Ako Group Ltd kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mawili na ofisi mbili za walimu katika shule ya msingi Kabale iliyopo katika kata ya Bulyanhulu halmashauri ya wilaya ya Msalala yakiendelea.

Na Kadama Malunde  - Malunde 1 blog
Kampuni ya Ako Group Limited inayotoa huduma ya chakula na usafi wa mazingira katika Mgodi wa Bulyanhulu imechangia vifaa vya ujenzi ikiwemo mifuko ya saruji, mawe, mbao, kokoto, nondo na fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi mbili kwenye shule ya Msingi Kabale iliyopo katika kijiji cha Kakola kata ya Bulyanhulu halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga.

Akikabidhi vifaa hivyo vya ujenzi, Februari 20,2021 Meneja wa Kampuni ya Ako Group Limited, Athanas Kahigi amesema Kampuni hiyo imeguswa na changamoto ya uhaba wa madarasa na ofisi za walimu katika shule ya msingi Kabale ambayo ina jumla ya wanafunzi 1980, madarasa saba na madawati 216.

“Leo tumekuja kukabidhi mifuko ya saruji 43,nondo 35,mawe tripu 10,kokoto tripu 10 na fedha shilingi 600,000/= kwa ajili ya fundi ujenzi vyote vimegharimu shilingi milioni 5. Na tunaahidi tutaendelea kupita hapa shuleni kuona ujenzi unavyoendelea,panapo upungufu tutachangia chochote ili kuinua boma hili”,amesema Kahigi.

Akifafanua zaidi Kahigi amesema kati ya mifuko 43 ya saruji mifuko 35 imetoka katika Kampuni ya Ako na mifuko nane imetoka kwa wadau wanaoshirikiana na Ako ambao wameamua kuishika mkono katika ujenzi wa madarasa na ofisi za walimu katika shule ya msingi Kabale.

“Kampuni yetu ya Ako Group Limited imekuwa na utaratibu wa kuchangia shughuli za maendeleo katika jamii inayotuzungumza kutekeleza matakwa ya kisheria. Mwezi Septemba 2020 pia tulichangia mifuko 200 ya saruji yenye thamani ya shilingi milioni 4.2 ili kusaidia ujenzi wa madarasa katika shule ya Msingi Bugarama iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Msalala”,ameongeza Kahigi.

Amebainisha kwa Kampuni ya Ako Group Limited inapenda kuona wanafunzi wanasoma katika mazingira rafiki hivyo kuahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika kuboresha sekta ya elimu

  Mratibu wa shughuli za maendeleo ya jamii wa Kampuni ya Ako Group Ltd, Mathias Mathias amesema ni wajibu wa Kampuni hiyo kushiriki kutatua changamoto zilizopo katika jamii na kwamba wataendelea kusaidia kwenye maeneo yenye changamoto.

Akipokea vifaa hivyo vya ujenzi, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala Dk. Ntanwa Kilagwire ameishukuru Kampuni ya Ako Group Ltd kwa kujitoa kuchangia katika sekta ya elimu na kuwaomba wadau wengine wajitokeze kusaidia kumaliza changamoto ya uhaba wa madarasa na madawati katika shule zilizopo katika halmashauri hiyo.

“Watoto hawa ni wetu, shule hizi ni zetu, niwaombe wadau,Makampuni yaliyopo katika eneo hili yasaidie. Haipendezi wanafunzi wakae chini wakati wazazi tupo”,amesema.

"Niwaombe pia wazazi muendelee na moyo huu mlioonesha kuanzisha ujenzi wa madarasa na ofisi za walimu katika shule hii ili wanafunzi wetu wapate mahali pa kusomea. Halmashauri itakuja kukamilisha ujenzi mkijenga boma”,ameongeza.

Naye Mbunge wa Jimbo la Msalala, Iddi Kassim Iddi ameishukuru Kampuni ya Ako Group Ltd kwa kuchangia ujenzi wa madarasa na ofisi za walimu huku akiiunga mkono kampuni hiyo kwa kuchangia Shilingi 450,000/= kwa ajili ya fedha za fundi ambapo Ako imetoa shilingi 600,000/= hivyo kukamilisha bajeti ya fundi ujenzi ambayo ni shilingi 1,050,000/=.

Diwani wa kata ya Bulyanhulu, Shija Joseph na Afisa Mtendaji wa kata ya Bulyanhulu Abdallah Kombo wameeleza kuwa kutokana na upungufu wa madarasa na ofisi za walimu katika shule ya msingi Kabale,waliamua kuyaomba makampuni yanayofanya shughuli zake katika eneo hilo wasaidie hivyo kuishukuru Kampuni ya Ako kwa kujitokeza kuwashika mkono.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kabale, Elias Kihamba amesema shule hiyo ina upungufu wa madarasa na ofisi ya walimu na kwamba shule hiyo ina wanafunzi 1980,walimu 12, madarasa 7 na madawati 216.

Nao wanafunzi wa shule hiyo,wamesema kukamilika kwa ujenzi wa madarasa hayo kutawapunguzia adha ya kujazana darasani.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Meneja wa Kampuni ya Ako Group Limited, Athanas Kahigi akizungumza akikabidhi vifaa vya ujenzi ikiwemo mifuko ya saruji, mawe, kokoto,mbao, nondo na fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi mbili kwenye shule ya Msingi Kabale iliyopo katika kijiji cha Kakola kata ya Bulyanhulu halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga Jumamosi Februari 20,2021. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja wa Kampuni ya Ako Group Limited, Athanas Kahigi akizungumza akikabidhi vifaa vya ujenzi ikiwemo mifuko ya saruji, mawe, kokoto,mbao, nondo na fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi mbili kwenye shule ya Msingi Kabale iliyopo katika kijiji cha Kakola kata ya Bulyanhulu halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga Jumamosi Februari 20,2021.
Meneja wa Kampuni ya Ako Group Limited, Athanas Kahigi akizungumza akikabidhi vifaa vya ujenzi ikiwemo mifuko ya saruji, mawe, kokoto, nondo na fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi mbili kwenye shule ya Msingi Kabale iliyopo katika kijiji cha Kakola kata ya Bulyanhulu halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga Jumamosi Februari 20,2021.
Mratibu wa shughuli za maendeleo ya jamii wa Kampuni ya Ako Group Ltd, Mathias Mathias akizungumza wakati Kampuni ya Ako Group Limited ikikabidhi vifaa vya ujenzi ikiwemo mifuko ya saruji, mawe, kokoto, nondo na fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi mbili kwenye shule ya Msingi Kabale iliyopo katika kijiji cha Kakola kata ya Bulyanhulu halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga Jumamosi Februari 20,2021.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala Dk. Ntanwa Kilagwire akizungumza wakati Kampuni ya Ako Group Limited ikikabidhi vifaa vya ujenzi ikiwemo mifuko ya saruji, mawe, kokoto, nondo na fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi mbili kwenye shule ya Msingi Kabale iliyopo katika kijiji cha Kakola kata ya Bulyanhulu halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga Jumamosi Februari 20,2021.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala Dk. Ntanwa Kilagwire akizungumza wakati Kampuni ya Ako Group Limited ikikabidhi vifaa vya ujenzi ikiwemo mifuko ya saruji, mawe, kokoto, nondo na fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi mbili kwenye shule ya Msingi Kabale iliyopo katika kijiji cha Kakola kata ya Bulyanhulu halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga Jumamosi Februari 20,2021.
Mbunge wa Jimbo la Msalala, Iddi Kassim Iddi akizungumza wakati Kampuni ya Ako Group Limited ikikabidhi vifaa vya ujenzi ikiwemo mifuko ya saruji, mawe, kokoto, nondo na fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi mbili kwenye shule ya Msingi Kabale iliyopo katika kijiji cha Kakola kata ya Bulyanhulu halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga Jumamosi Februari 20,2021.
Meneja wa Kampuni ya Ako Group Limited, Athanas Kahigi (wa pili kulia) akiwakabidhi viongozi wa kamati ya shule ya Msingi Kabale iliyopo katika kata ya Bulyanhulu shilingi 600,000 kwa ajili ya fundi ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi mbili kwenye hiyo.
Meneja wa Kampuni ya Ako Group Limited, Athanas Kahigi (wa tatu kulia) akiwakabidhi viongozi wa halmashauri ya Msalala sehemu ya mifuko 43 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi mbili kwenye shule ya Msingi Kabale iliyopo katika kijiji cha Kakola kata ya Bulyanhulu halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga Jumamosi Februari 20,2021.
Meneja wa Kampuni ya Ako Group Limited, Athanas Kahigi (wa nne kulia) akiwakabidhi viongozi wa halmashauri ya Msalala sehemu ya nondo na mbao kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi mbili kwenye shule ya Msingi Kabale iliyopo katika kijiji cha Kakola kata ya Bulyanhulu halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga Jumamosi Februari 20,2021.
Meneja wa Kampuni ya Ako Group Limited, Athanas Kahigi (katikati) akiwakabidhi viongozi wa halmashauri ya Msalala sehemu ya mawe kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi mbili kwenye shule ya Msingi Kabale iliyopo katika kijiji cha Kakola kata ya Bulyanhulu halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga Jumamosi Februari 20,2021.
Sehemu ya vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na Kampuni ya Ako Group Limited kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi mbili kwenye shule ya Msingi Kabale iliyopo katika kijiji cha Kakola kata ya Bulyanhulu halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga.
Sehemu ya vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na Kampuni ya Ako Group Limited kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi mbili kwenye shule ya Msingi Kabale iliyopo katika kijiji cha Kakola kata ya Bulyanhulu halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga.
Sehemu ya mifuko ya saruji iliyotolewa na Kampuni ya Ako Group Ltd.
Ujenzi wa vyumba vya madarasa mawili na ofisi mbili za walimu katika shule ya msingi Kabale ukiendelea
Wazazi na walezi wakiwa katika shule ya msingi Kabale
Diwani wa kata ya Bulyanhulu, Shija Joseph (katikati) akishirikiana na wananchi kubeba mfuko wa saruji
Diwani wa Viti Maalum Nyangwene Mnyirwa (kushoto) akishirikiana na wananchi kubeba mfuko wa saruji
Afisa Mtendaji wa kata ya Bulyanhulu Abdallah Kombo akizungumza wakati Kampuni ya Ako Group Limited ikikabidhi vifaa vya ujenzi ikiwemo mifuko ya saruji, mawe, kokoto, nondo na fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi mbili kwenye shule ya Msingi Kabale
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kabale, Elias Kihamba akizungumza wakati Kampuni ya Ako Group Limited ikikabidhi vifaa vya ujenzi ikiwemo mifuko ya saruji, mawe, kokoto, nondo na fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi mbili kwenye shule ya Msingi Kabale
Diwani wa kata ya Bulyanhulu, Shija Joseph akizungumza wakati Kampuni ya Ako Group Limited ikikabidhi vifaa vya ujenzi ikiwemo mifuko ya saruji, mawe, kokoto, nondo na fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi mbili kwenye shule ya Msingi Kabale
Wazazi wakifuatilia matukio wakati Kampuni ya Ako Group Limited ikikabidhi vifaa vya ujenzi ikiwemo mifuko ya saruji, mawe, kokoto, nondo na fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi mbili kwenye shule ya Msingi Kabale
Wanafunzi wakifuatilia matukio wakati Kampuni ya Ako Group Limited ikikabidhi vifaa vya ujenzi ikiwemo mifuko ya saruji, mawe, kokoto, nondo na fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi mbili kwenye shule ya Msingi Kabale
Wazazi wakifuatilia matukio wakati Kampuni ya Ako Group Limited ikikabidhi vifaa vya ujenzi ikiwemo mifuko ya saruji, mawe, kokoto, nondo na fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi mbili kwenye shule ya Msingi Kabale
Wazazi wakifuatilia matukio wakati Kampuni ya Ako Group Limited ikikabidhi vifaa vya ujenzi ikiwemo mifuko ya saruji, mawe, kokoto, nondo na fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi mbili kwenye shule ya Msingi Kabale.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post