Katibu mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) yenye makao yake makuu mjini Moshi, Arthur Shoo enzi za uhai wake
Katibu mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) yenye makao yake makuu mjini Moshi, Arthur Shoo
***
Katibu mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) yenye makao yake makuu mjini Moshi, Arthur Shoo amefariki dunia katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC alikokuwa akipatiwa matibabu.
Mkuu wa Dayosisi hiyo ambaye ndiye mkuu wa Kanisa hilo Tanzania, Askofu Fredrick Shoo amesema kuwa mtendaji wake huyo mkuu alifariki dunia jana usiku akiendelea na matibabu hospitali ya KCMC na kueleza kuwa alikuwa amelazwa katika hospitali hiyo inayomilikiwa na Shirika la Msamaria Mwema (GSF) tangu Jumatatu ya wiki hii.