MBUNGE NEEMA LUGANGIRA AHOJI MAHUSIANO KATI YA LISHE BORA NA VIFO VYA AKINA MAMA WAJAWAZITO VINAVYOTOKANA NA UZAZI

 

Mkutano wa "Tanzania Maternal Mortality and Nutrition - Mama Mjamzito na Mbogamboga" ambao umeandaliwa na Mbunge Neema Lugangira ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani ukiendelea
Mkutano wa "Tanzania Maternal Mortality and Nutrition - Mama Mjamzito na Mbogamboga" ambao umeandaliwa na Mbunge Neema Lugangira ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani ukiendelea

MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia NGOs Mhe Neema Lugangira ameandaa mkutano wa "Tanzania Maternal Mortality and Nutrition - Mama Mjamzito na Mbogamboga"

 
Mkutano huo ulilenga kujadiliana kuhusu uhusiano kati ya vifo vya wakina mama wajawazito wanapojifungua na lishe bora kwa maana ya upungufu wa damu "Anemia".

Katika mkutano huo zaidi ya watu 50 walishiriki kupitia Mtandao wa Zoom ambapo watoa mada waliwakilisha makundi muhimu . 

Watoa mada waliwakilisha makundi muhimu kama Dr. Grace Moshi - Msimamizi wa Masuala ya Lishe; Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Dr. Lilian Mnabwiru - Katibu; Chama Cha Madaktari Tanzania huku Anna Sengoka wa Chama Cha Wakunga Tanzania naye akiwasilisha mada.

 Pia katika mkutano huo uliwashirikisha Dr. Ali Said - Daktari Bingwa wa Masuala ya Wanawake na Mwalimu MUHIMBILI na Dr. Isihaka Mwandalima - Mkurugenzi (Technical) - Shirika lisilo la Kiserikali (NGO); Pathfinder International

 Mkutano huu uliendeshwa na Wenyeviti Wawili Mhe Neema Lugangira (Mb.) na Dr. Frank Minja; Rais wa Diaspora ya Watanzania wanaoishi Marekani.

Akizungumza baada ya mkutano Mbunge Neema Lugangira alisema ni  dhahiri mkutano huu wa kwanza kwa hakika umedhihirisha umuhimu wa lishe bora kwa mama mjamzito kabla, wakati na baada ya kujifungua. 

Mhe Mbunge alipoulizwa nini mchango wake katika kufanikisha suala hilo, alisema kuwa Shirika la Agri Thamani Foundation ambalo yeye ni Mkurugenzi lipo mstari wa mbele kuhamasisha ulaji wa matunda na mbogamboga ngazi ya kaya hususan kwa vijana balehe.
 
Alieleza ndio maana shirika hilo limekuja na programu ya kutoa msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike wa sekondari huku msaada huu ukiendana na elimu ya lishe bora ikiwemo kuanzisha bustani za mfano za mbogamboga shuleni na kaya.

Hata hivyo Mhe Neema alisema ni dhamira yake kuendelea kuandaa mijadala ya namna hii kwa njia mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha ajenda ya lishe bora inapata kipaumbele inachostahili".



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post