DK. AKWILAPO AIPONGEZA CSSC KWA KUTOA ELIMU BORA NCHINI...ASEMA SERIKALI ITAYAFANYIA KAZI MAONI YENU

 

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Taknolojia Dkt Leonard Akwilapo akizungumza wakati akifungua Mkutano wa wakuu wa shule za Sekondari na Msingi za Makanisa yaliyo chini ya Kanisa Katoliki na Jumuiya ya Kikristo Tanzania ambayo yanaratibiwa na Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) iliyofanyika leo Januari 25,2021 jijini Dodoma.

Wakuu wa Shule wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Taknolojia Dkt Leonard Akwilapo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa wakuu wa shule za Sekondari na Msingi za Makanisa yaliyo chini ya Kanisa Katoliki na Jumuiya ya Kikristo Tanzania ambayo yanaratibiwa na Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) iliyofanyika leo Januari 25,2021 jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) Bw.Peter Maduki,akielezea jinsi wanavyotoa elimu katika shule zao wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa wakuu wa shule za Sekondari na Msingi za Makanisa yaliyo chini ya Kanisa Katoliki na Jumuiya ya Kikristo Tanzania ambayo yanaratibiwa na Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) iliyofanyika leo Januari 25,2021 jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa huduma za Elimu wa Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) Mwl.Petro Pamba,akitoa taarifa kwenye Mkutano wa wakuu wa shule za Sekondari na Msingi za Makanisa yaliyo chini ya Kanisa Katoliki na Jumuiya ya Kikristo Tanzania ambayo yanaratibiwa na Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) iliyofanyika leo Januari 25,2021 jijini Dodoma.

Mwalimu Deogratius Renatus kutoka Sekondari ya St.Galgan kutoka Arusha akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi mara baada ya kufungua Mkutano wa wakuu wa shule za Sekondari na Msingi za Makanisa yaliyo chini ya Kanisa Katoliki na Jumuiya ya Kikristo Tanzania ambayo yanaratibiwa na Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) iliyofanyika leo Januari 25,2021 jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakifatilia Hotuba ya Mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa wakuu wa shule za sekondari na Msingi za Makanisa yaliyo chini ya Kanisa Katoliki na Jumuiya ya Kikristo Tanzania ambayo yanaratibiwa na Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC)

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Taknolojia Dkt Leonard Akwilapo akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kufungua Mkutano wa wakuu wa shule za Sekondari na Msingi za Makanisa yaliyo chini ya Kanisa Katoliki na Jumuiya ya Kikristo Tanzania ambayo yanaratibiwa na Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) iliyofanyika leo Januari 25,2021 jijini Dodoma.


Na Alex Sonna,Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk.Leonard Akwilapo, ameipongeza Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii(CSSC),kwa mchango wake katika sekta ya elimu nchini huku akiahidi serikali kufanyia kazi maoni yanayotolewa ikiwamo kupunguza kwa mitihani ya majaribio.

Akifungua leo Mkutano wa mwaka cha Wakuu wa Shule za Sekondari na Msingi za makanisa, Dk.Akwilapo, amesema suala la mitihani ya majaribio lina utata na kudai kuwa ni mingi na wakati mwingine inaipa Wizara wakati mgumu kuiratibu.

“Kuna wengine wanadhani elimu inapatikana kwa kuuliza wanafunzi maswali mara kwa mara, ili ng’ombe anenepe ni kuhakikisha amekula na si kumpima uzito asubuhi, mchana na jioni, kitu kizuri ni kuimarisha ufundishaji,”amesema.

Ameongeza kuwa “Kuna dhana nyingine imeongezeka hadi kuweka kambi kufanyishwa mitihani kila siku hadi jumamosi,kuna mambo tumekemea na si sahihi kwamba ili mwanafunzi afaulu ni kupigwa mitihani, majaribio hatuyakatai bali kila mara inamchosha mtoto.”

Aidha, amesema nia ya serikali ni kutoleta mgongano na wanaendelea na majadiliano na kutaka kuimarisha ufundishaji na si kupewa mitihani kila siku.

Pia amezitaka shule kuzingatia maelekezo ya serikali katika kumkaririsha mwanafunzi darasa kwa kuwa suala hilo linalalamikiwa.

“Tunatambua mchango wenu mnaoutoa nchini katika sekta ya elimu, hata hivyo baadhi ya shule zisizo za serikali kama nyingine zipo kwenu au hazipo, ambazo zinaenda kinyume na maelekezo ya serikali, niwakumbushe myazingatie kukaririsha wanafunzi bila kuzingatia taratibu ni tatizo tunalokutana nalo sana,”amesema.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Tume hiyo, Peter Maduki, amesema la mkutano huo ni kuweka mikakati ya utoaji huduma bora ya elimu na kuangalia kero zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi.

“Pia tutajadili namna ya kuboresha huduma ya TEHAMA itatusaidia sana katika kuboresha elimu na kupunguza gharama ya utoaji wa elimu na kuwapunguzia mzigo wazazi,”amesema.

Ameomba Wizara kuangalia namna ya kupunguza mitihani ya majaribio ambayo imeonekana kuendelea kuibuka mbali na inayopaswa kufanyika kitaifa.

“Kunaendelea kuibuka mitihani ya majaribio mara ya kikata, kiwilaya hali inayosababisha mwingiliano wa mitihani na hii hata inashusha ubora wa mitihani tunaomba umakini zaidi uwepo katika kuendesha mitihani,”amesema.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments