WHATSAPP NA FACEBOOK ZAWALAZIMISHA WATUMIAJI KUTUMA MAELEZO YAO BINAFSI


WhatsApp inawalazimisha watumiaji wake kukubali iwasilishe maelezo yao binafsi kwa Facebook ikiwa wanataka kuendelea kutumia huduma hiyo.

Kampuni hilo inawaonya watumiaji kupitia taarifa zinazotolewa kwenye simu zao zinazosema "unahitajika kuruhusu agizo hili ili kuendelea kutumia WhatsApp" - au wafute akaunti zao.

Lakini Facebook, ambayo inamiliki WhatsApp, imesema watumiaji wa mtandao huo waliopo Ulaya na Uingereza hawataathiriwa na muongozo huo na watahitajika kukubali masharti mapya.

Hatua hiyo imeungwa mkono na baadhi ya watu wakisema ni ushindi kwa wasimamizi wa faragha wa EU.

Muda wa mwisho wakukubali mabadiliko hayo mapya katika maeneo hayo ni Februari 8, na baada ya hapo "utahitajika kukubali agizo hilo ili kuendelea kutumia WhatsApp", kampuni hiyo ilisema katika taarifa zinazowasilishwa kwa watumiaji.

Sehemu ya sera ya faragha ya kimataifa ya awali ambayo ilikuwa inawasihi watumiaji kukubali maelezo yao kuwasilishwa kwa Facebook kwa hiari katika siku 30 za kwanza imeondolewa baada ya mabadiliko haya mapya kuanza kutekelezwa.

Badala ya katika maagizo ya hivi punde, watumiaji wanaelekezwa sehemu ya kutafuta msaada mtandaoni "ikiwa wangelipendelea kufuta akaunti zao".

Hatua hiyo imewafanya baadhi ya watu mitandaoni - akiwemo mwanzilishi wa Tesla na SpaceX Elon Musk- kutoa with kwawatumiaji wa mtandao huo kujiunga na huduma zingine za ujumbe wa faragha kama Signal na Telegram.

Kutojumuishwa kwa Ulaya

Awali kulikuwa na mkanganiyiko kuhusu jinsi ya hatua hiyo itawaathiri watumiaji wa Ulaya na Uingereza.

Muktasari wa ''maelezo muhimu'' ya mabadiliko hayo mapya yatajumuishwa na Facebook kimataifa - lakini hatua hiyo haijajumuishwa katika huduma sawa na hiyo kwa watumiaji wa mtandao huo yaliyopo Ulaya.

Baadaye Alhamisi, Facebook ilitoa taarifa ikisema kwamba mabadiliko hayo hayahusu" eneo la Ulaya" - ambayo inajumuisha EU, EEA na Uingereza baada ya -Brexit.

"Ili kuondoa shaka, katika mpango huu mpya WhatsApp haiwasilishi data ya watumiaji wake wa maeneo ya Ulaya kwa Facebook kwa lengo la Facebook kutumia data hiyo kujiimarisha au kwa ajili ya biashara" msemaji alisema.

Hata hivyo, toleo jipya la sera ya faragha kwa watumiaji wa Ulaya inasema wazi kuwa data inaweza kutumiwa na kampuni zingine za Facebook kuonesha matangazo ya kibinafsi na ofa, kutoa maoni kuhusu maudhui na ''kusaidia'' katika kukamilisha mauzo miongoni mwa sababu zingine.

Facebook inasema haitumii maelezo ya WhatsApp kwa sababu kama hizo za Ulaya, kwa sababu ya mazungumzo iliyofanya na mashirika ya kulinda usalama wa maelezo binafsi.

Wengine walisifia hatua hiyo kuchangia ufanisi wa kimaendeleo kutokana na masharti makali yaliyobuniwa kuhusu faragha ya mtu binafsi katika miaka ya hivi karibuni.

Facebook inajipatia haki ya kufikia data zetu zote za WhatsApp isipokuwa…. Kwa wale wanaoishi EU.

"Ndio maana ulinzi wa data ni muhimu."

Ni maelezo gani yanayokusanywa?
Maelezo ya aina ya data inayokusanywa na WhatsApp - na ambayo sasa inawasilishwa kwa Facebook na ambayo haijumuishi watumiaji wa Ulaya - hufichwa katika hati rasmi zinazounda sheria na sera ya faragha.

Katika ujumbe wa maswali na majibu WhatsApp ilisema inashirikisha habari ya watumiaji wake na kampuni zingine za Facebook, ikiwa ni pamoja na:

•Nambari ya simu na maelezo mengine yanayotolewa wakati wa usajili (kama vile jina)

•Maelezo kuhusu simu yako, ikiwemo aina ya simu na kampuni ya simu

•Anuani ambayo inaonesha mahali pa unganisho lako la mtandao

•malipo yoyote na shughuli za kifedha zilizofanywa kupitia WhatsApp

Lakini pia ilisema kuwa huenda ikashirika data inayojumuishwa katika sera yake ya faragha - ambayo inaweza kujumuisha anwani, taarifa mpya za mtumiaji (status updates), wakati watu wanatumia WhatsApp na kwa muda gani, na nambari za kipekee za kutambua simu za watumiaji.

Facebook haijajibu ombi la kutaka ifafanue kwa nini iliamua kufanya ghafla mabadiliko hayo.

 CHANZO - BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post