WAZIRI MKUU WA DRC AJIUZULU | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, January 30, 2021

WAZIRI MKUU WA DRC AJIUZULU

  Malunde       Saturday, January 30, 2021
Sylvestre Ilunga Ilunkamba amejiuzulu rasmi kama waziri mkuu wa Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo, na kuwasilisha barua yake kwa Rais FĂ©lix Tshisekedi.

Bw Ilunga, ambaye ni mshirika mkuu wa mtangulizi wa Rais Tshisekedi, Joseph Kabila, ameongoza baraza la mawaziri la serikali ya Muungano kwa miezi 15.

Hata hivyo wabunge walipitisha kura ya kutokuwa na Imani na serikali yake Jumatano wiki hii na akapewa saa 24 awe amejiuzulu.

Kujiuzulu kwake kunatoa fursa kwa Rais Tshisekedi ya kuwateua washirika wake kama mawaziri.

Hadi sasa, utendaji wa Bw Tshisekedi umekuwa ukidhibitiwa na, muungano alionao na Bw Kabila ambao uliafikiwa wakati alipoingia madarakani miaka miwili iliyopita.

Ushindi wake katika uchaguzi mwezi Disemba 2018 ulisifiwa kama wa kihistoria-ambapo kulikuwa na makabidhiano ya kwanza ya utawala kwa njia ya amani ambayo hayakuwahi kushuhudiwa katika historia ya miongo sita nchini humo.

Bw Tshisekedi bado hajamchagua waziri mkuu mpya,ambaye ataunda serikali ijayo.

 CHANZO - BBC SWAHILI

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post