Tazama Picha : DONALD TRUMP AONDOKA IKULU BIDEN AKIAPISHWA KUWA RAIS WA MAREKANI


Rais wa Marekani Donald Trump ameondoka Ikulu ya Marekani akiwa sambamba na mkewe, Melania Trump.

Wawili hao walielekea kambi ya jeshi, huko Maryland ambapo sherehe za mwisho kuwaaga zinafanyika.

Baada ya shughuli hiyo Rais Trump atasafiri mpaka Florida kwa ndege ya Air Force One, na ataishi katika makazi yake ya kifahari ya la Mar-a-Lago

Katika hatua nyingine Makamu wa Rais , Mike Pence, hatakuwepo kwenye sherehe za kumuaga Trump isipokuwa atahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Biden na Harris baadae hii leo.

Akitoa maneno mafupi kwa wanahabari kabla ya kuondoka, Rais Trump amesema Ikulu palikuwa makazi mazuri sana.

''Tumekuwa na miaka minne mizuri sana na tumefanikisha mengi,'' alisema Trump.

''Tunawapenda Wamarekani na kimekuwa kitu cha kipekee'', aliongeza.
'Tulipigwa sana'

Rais Trump amegusia kuhusu Janga la corona- ambalo lilishika kasi katika kipindi cha miezi tisa iliyopita ya utawala wake

''Tulifanya jambo ambalo ni muujiza wa kitabibu nalo ni chanjo,'' alisema.

Amesema kirusi ni ''kitu kibaya sana'' na kwa mara nyingine aliita ''kirusi cha China'' lakini ametoa ''salamu za upendo'' kwa familia zilizoathirika kwa kiasi kikubwa.

Vifo vilivyotokana na Covid-19 nchini humo sasa ni zaidi ya 400,000, na idadi ya vifo imeendelea kuongezeka

Trump awatakia 'mafanikio mema' warithi wake

Akihitimisha hotuba yake, Rais Donald Trump amesema imekuwa "heshima kubwa " kuwa rais. Akiwahutubia wafuasi, amesema "atawapigania kila wakati" na atakuwa "akiangalia na kusikiliza" na anaahidi kurudi kwa kiasi fulani.

Ameutakia pia uongozi mpya "mafanikio makubwa" kwa siku zijazo - lakini hakuwataja Joe Biden au Kamala Harris kwa majina.

Ndege ya Marine One katika Ikulu ya Whitehouse ikimsubiri kumsafirisha rais Donald Trump
Ndege ya Marine One ikitua katika Ikulu ya Whitesoue huku rais Trump akisubiri
Akizungumza na wanahabari muda mfupi kabla ya kupanda ndege ya Marine One , rais Trump alisema kwamba Ikulu ya Whitehouse ilikuwa nyumba bora zaidi duniani
Rais Donald Trump na Mkewe Melania Trump wakiondoka katika Ikulu ya Whitehouse
Trump na mkewe Melania Trump akielekea kupanda ndege ya Marine One
Ndege ya Marine One katika ikulu ya Whitehouse
Ndege ya Marine One ilipokuwa ikiondoka katika ikulu ya Whitehouse

CHANZO - BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post