AWAUA WAZAZI WAKE, NDUGU NA MFANYAKAZI WA NDANI AKIDAI KUBAGULIWA KWENYE FAMILIAKijana Lawrence Waruinge (kushoto) na mpenzi wake (kulia)
**
Lawrence Waruinge na mpenzi wake wamefikishwa mbele ya makahakama Kaunti ya Kiambu, Kenya, kutokana na mauaji ya watu watano wote wa familia ya Lawrence, akiwemo baba yake mzazi, mama yake mzazi, ndugu zake wawili pamoja na mfanyakazi wa ndani.

Mauaji hayo anatuhumiwa kutekeleza Lawrence wiki iliyopita na amekiri kuyatekeleza mauaji hayo. Baada ya kukiri, sasa siku ya Alhamisi Januari 14, 2021, atafanyiwa uchunguzi wa akili kabla ya kesi yake kuanza.

Baada ya kukiri kutekeleza unyama huo Lawrence aliwapeleka maafisa wa upelelezi hadi pale alipoficha vifaa alivyotumia kwenye mauaji hayo, akisema kuwa aliamua kuchukua hatua hiyo, kutokana na kile alichokitaja kama kubaguliwa na familia yake.

Kijana huyu mwenye umri wa miaka 22, atafikishwa tena mahakamani tarehe 25 mwezi huu baada ya uchunguzi kukamilika, pamoja na mpenzi wake, anayesemekana kukodisha chumba walichotorokea kabla na baada ya maujaji, wote wakishtakiwa kwa kosa la mauaji.

 Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments