Tanzia : BILLIE EDMOTT AFARIKI DUNIA


Billie Edmott enzi za uhai wake.

Afisa Misitu na Utunzaji Mazingira Mwandamizi mkoa wa Shinyanga, Billie Edmott amefariki dunia.

Kwa Mujibu wa taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Lubaga Farm kata ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga Joachim Jeremia amesema Billie Edmott amekutwa amefariki dunia ndani ya nyumba yake leo Jumanne Januari 12, 2021 mchana.

 Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela amethibitisha taarifa kuhusu kifo cha Billie Edmott.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post