WAZIRI WA MADINI DOTTO BITEKO AMVUA MADARAKA MWENYEKITI WA SOKO LA MADINI CHUNYA


Waziri wa Madini Dotto Biteko

Waziri wa Madini Dotto Biteko, leo Desemba 14, 2020, amemvua madaraka Mwenyekiti wa Soko la Madini Chunya, pamoja na kuwasimamisha kazi wafanyakazi wengine watatu.

Biteko amefanya maamuzi hayo leo alipotembelea soko hilo katika ziara yake anayoendelea nayo, ikiwa ni siku chache tangu ateuliwe na kuapishwa kuitumikia Wizara hiyo, ambapo amesema Mwenyekiti huyo amekuwa na uzembe kiasi cha madini kutoroshwa.

Aidha Waziri Biteko pia amefuta leseni za wachimbaji watano ambao wamevunja taratibu mbalimbali pamoja na ameagiza mawakala na wanunuzi wa dhahabu watatu kukamatwa kwaajili ya kuchukuliwa hatua.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amemwagiza RPC kuwakamata wahusika wote na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria mara moja.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments