Tanzia : MSANII WA FILAMU MZEE JENGUA AFARIKI DUNIA


Mzee Jengua enzi za uhai wake

Chama cha waigizaji Dar es Salaam Tanzania, kimetangaza kifo cha msanii maarufu wa filamu Mohammed Funga Funga maarufu Mzee Jengua ambaye amefariki dunia siku ya leo Disemba 15 majira ya asubuhi nyumbani kwa mtoto wake Mkuranga.

Taarifa iliyotolewa na katibu wa chama cha waigizaji Mkoa wa Dar es Salaam, Doricy Kente inaeleza kuwa mke wa msanii huyo amethibitisha kifo hicho na taarifa kuhusu mipango ya mazishi wanasubiria vikao vya familia ili kutoa ratiba kamili ya mazishi hayo.

"Taarifa tumezipokea tunasubiria vikao vya familia yake ili tukampumzishe mzee wetu, unapotamka Jengua unakuwa umetaja jina kubwa sana kwenye soko la filamu hapa nchini Tanzania, alikuwa mcheshi sana,ukimuangalia hachoshi na ana vituko vingi, mimi nimecheza naye filamu moja ya Mke mwema na alikuwa kama baba mkwe wangu", ameeleza Msanii wa filamu Steve Nyerere

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post