WEMA SEPETU AZUA GUMZO BAADA YA KUMPELEKA MBWA WAKE SALUNI


Msanii wa filamu Wema Sepetu na Mbwa wake Vanilla Nunu


Staa wa filamu hapa nchini Tanzania Wema Sepetu amezua jambo kwa wanazengo wa mtandao wa Instagram baada ya kufunguka kuwa huwa anampeleka saluni mbwa wake aitwaye Vanilla Nunu angalau mara mbili kwa mwezi.

Wema Sepetu ame-post picha hiyo ya mbwa wake wa kike kisha kuandika maneno ya kiingereza ambayo kwa kiswahili yanatafsirika kama "Mtoto wangu amefurahia siku yake ya saluni leo, ndiyo huwa anaenda saluni mara mbili kwa mwezi" 

Baada ya kupost picha ya mbwa wake huyo ambaye ana wafuasi elfu 10 kwenye mtandao huo, comments zimekuwa nyingi kwa watu wa jamhuri ya instagram ambapo wameshambulia Wema Sepetu kwa kushea habari hiyo.

Sasa hizi hapa ni baadhi ya comments hizo "Vanilla Nunu anatushinda urembo ndugu yangu, wewe saloon hadi lilie lamgambo" Mac 

"Utaishia kuwa na baby hao hao ndiyo maana muda mwingine Mungu anashindwa kuwasaidia kwa sababu ya uzungu mwingi usio na maana, ina maana mwanao kawa mbwa sasa" Izack Tz 

"Si afadhali ukachukue watoto yatima huko, unafeli sana yaani" Salma Likokwe

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post