Tanzia : KADA WA CCM EGLA MAMOTO AFARIKI DUNIA....UVCCM YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI

 Aliyewahi kuwa Kaimu Katibu idara ya Uhamasishaji na Chipukizi wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Egla Mamoto amefariki dunia.

Mamoto ambaye katika uchaguzi wa mwaka huu aligombea ubunge kupitia kundi la wazazi, amefariki katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma alikokimbizwa kwa matibabu baada ya kujisikia vibaya usiku wa kuamkia leo Jumapili Desemba 27, 2020.

Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi wa UVCCM Taifam Leonard Singo ametoa taarifa iliyoeleza kuwa Mamoto aliugua ghafla.

Singo amesema marehemu alikuwa hazina katika kipindi cha uhai wake na kuwa hakupenda kuona CCM kinashindwa katika uchaguzi wowote.

Katika uhai wake alikaimu Katibu wa uhamasishaji Taifa katika kipindi cha mwaka mmoja 2015/16 ambapo katika kipindi hicho alikuwa mjumbe wa Baraza Kuu la Vijana wa Uvccm.

Baadhi ya watu ambao wapo katika kundi moja la WhatsApp wamesema hadi saa nne usiku wa kuamkia leo Mamoto alikuwa akichati kwenye kundi hilo akiwatakia watu maisha mema na kumaliza mwaka salama.Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post