SONY MUSIC AFRICA YAMTEUA CHRISTINE ‘SEVEN’ MOSHA KUONGOZA KITENGO CHA MASOKO NA MAENDELEO YA WASANII UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI


Sony Music Entertainment Africa imemteua Christine Mosha, anayejulikana zaidi kama ‘Seven’, kuongoza kitengo cha Masoko na Maendeleo ya Wasanii katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Akianza kazi rasmi, Mosha atajenga orodha ya kampuni ya vipaji vya eneo hilo na kukuza kazi zake za kimataifa na zilizopo katika eneo hilo kutokea makazi yake nchini Tanzania. Ataripoti moja kwa moja kwa Sean Watson, Mkurugenzi Mtendaji, Sony Music Africa.

“Seven ametumia maisha yake mengi kuchangia katika tasnia ya burudani ya Afrika. Ni mtetezi mwenye mapenzi makubwa katika kila kitu ambacho Afrika Mashariki inaweza kuipa dunia,” amesema  Sean Watson, Mkurugenzi Mtendaji,  Sony Music Africa.

“Kwa miaka kadhaa tayari amekuwa mshirika muhimu kwetu, akitupa utambuzi wa kipekee wa njia sahihi za kufanya kazi Afrika Mashariki, ambako ni kitovu chenye nguvu na kilichochangamka kwa muziki barani. Hivyo tumefurahi kuwa naye, akisaidia kupanua orodha yetu ya wasanii wa Afrika Mashariki na kuonesha mkusanyiko wetu wa kazi za kimataifa kwenye hadhira mpya.”

“Sony Music ina historia kubwa kwenye tasnia ya muziki duniani, kwahiyo kuwa sehemu ya kampuni hii katika wakati huu wa kazi yangu inaonekana ni toshelezo zuri ambapo nitaleta uzoefu na utalaamu wangu kibiashara kwenye kampuni nzima,” ameongeza Mosha. “Nimefurahia sana kuhusu kujiunga na Sony Music Africa, natazamia kuendelea kuleta matokeo chanya kwenye tasnia ya burudani, sio tu Afrika Mashariki bali katika bara zima.”

Mosha analeta uzoefu wa miaka 15 katika tasnia ya muziki ya Afrika katika kazi hiyo na amekuwa akifanya kazi kwa ukaribu na Sony Music Africa kwa miaka mingi. Mwaka 2017 alianzisha lebo yake binafsi ya muziki na kampuni ya kusimamia vipaji, Rockstar Africa, ambako alichochea mafanikio kibiashara kwa wasanii wengi wa muziki wa Afrika Mashariki wakiwemo Lady Jaydee, Ray C, TID, Rose Muhando, Xtatic, Alikiba na Ommy Dimpoz. Tangu 2010, Mosha ameiongoza pia ROCKSTAR 4000 MUSIC ENTERTAINMENT, kampuni ya kwanza ya muziki ya Afrika inayojitegemea pamoja na mtandao wa utayarishaji wa maudhui, kidigitali na matukio.

Huko, alisimamia uchapishaji wa muziki, mikataba ya muziki na leseni za maudhui akiwa na Sony Music Africa, ikiwemo kufanya kazi kwenye kampeni kwaajili ya kombe la dunia la FIFA 2010 lililofanyika Afrika Kusini.

Mosha alianza kazi yake mwaka 2006 kama mtangazaji wa redio wa kipindi cha asubuhi, promota na gwiji wa masoko Clouds Media Group, shirika la habari linaloongoza Tanzania kabla ya kuhamia MTV mwaka 2005, ambako aliongoza kitengo cha wasanii na kazi pamoja na biashara barani Afrika, alizindua kituo cha MTV Base Tanzania, na akifanya kazi kwenye miradi ikiwemo Staying Alive Campaign akiwa na Kelly Rowland nchini Tanzania pamoja na ziara ya Water for Life iliyoshirikisha Umoja wa Mataifa, Clouds Media na Jay Z.

Katika miaka mitano iliyofuata hadi alipoanzisha Rockstar Africa, Mosha alikuza orodha ya kazi alizofanya kuwajumuisha wasanii kama Alikiba (Best African Act katika MTV Europe Music Awards mwaka 2016) na Ommy Dimpoz (Best Male East Africa katika tuzo za AFRIMA mwaka 2019), pamoja na watayarishaji wa muziki, wanamichezo na waigizaji.

MWISHODownload/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post